RC KUNENGE AWAASA WAHITMU KADA YA AFYA KUZINGATIA MAAFILI


Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhe Abubakar Kunenge amewataka wahitimu kada ya afya kuhakikisha wanasimamia maadili ya kazi yao kutokana na kazi yao kushughulikia zaidi na maisha ya watu.

Mhe.Kunenge ameyasema hayo leo Julai, 30 2021 alipohudhuria mahafali ya 54 ya chuo cha Tiba na Sayansi Shirikishi kilichopo Kibaha.

"Katika taaluma ambazo mtumishi anatakiwa kuwa na nidhamu ni hii ya afya kwasababu mnashughulika zaidi na afya  maisha ya watu hakika hapa mnatakiwa kuwa na maadili" alisema.

Alisema anahitaji kuona wahitimu hao wakisifiwa kwa kuwa na nidhamu katika maeneo watakayoenda kufanya kazi na kwamba hiyo itakuwa heshima kwake 

Katika mahafaali hayo wahitimu 94 walikabidhiwa vyeti vya kuhitimu na Mh. Kunenge.



 

Comments

Popular posts from this blog

CV YA KOCHA MPYA WA SIMBA PABLO FRANCO MARTIN "USIPIME"