WAKATI UMEFIKA KUUNDWA TUME YA KUPAMBANA NA UDHALILISHAJI KIJINSIA ZANZIBAR: RAIS MWINYI


RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akihutubia na kulifungua Kongamanbo la Harakati la Kutokomeza Vitendo vya Udhalilishaji Zanzibar,Tulipotoka,Tulipo na Tunakokwenda, lililofanyika katika ukumbi wa Sheikh Idrisa Abdul Wakil Kikwajuni Jijini Zanzibar, lililoandaliwa na Jumuiya na Wanasheria Wanawake Zanzibar.(ZAFELA) (Picha na Ikulu
BAADHI ya Wananchi wakifuatilia hutuba ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi (hayupo pichani) akihutubia na kulifungua Kongamano la Harakati za Kutokomeza Vitendo vya Udhalilishaji Zanzibar lililofanyika katika ukumbi wa Sheikh Idrisa Abdulwakil Kikwajuni Jijini Zanzibar.(Picha na Ikulu)
BAADHI ya Mawaziri wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar wakifuatilia hutuba ya ufunguzi wa Kongamano la Harakati za Kutokomeza Vitendo vya Udhalilishaji Zanzibar, wakati Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi.(hayupo pichani)  akihutubia na kulifungua katika ukumbi wa Sheikh Idrisa Abdulwakil Kikwajuni Jijini Zanzibar.(Picha na Ikulu)
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi, akimsikiliza Kiongozo wa Kikundi cha Yataka Moyo cha Kajengwa Makunduchi Bi. Sinajambo Mkonde akitowa maelezo ya bidhaa zinazozalishwa na kikundi hicho wakati alipotembelea mabanda ya maonesho ya Wajasiriamali Wanawake Waliowezeshwa na (ZAFELA) wakati wa hafla ya ufunguzi wa Kongamano la Harakati za Kutokomeza Vitendo vya Udhalilishaji Zanzibar, lililofanyika katika ukumbi wa Sheikh Idrisa Abdulwakil Kikwajuni Jijini Zanzibar na (kulia kwa Rais) Mwenyekiti wa Jumuiya wa Wanasheria Wanawake Zanzibar (ZAFELA) Bi. Safia Hija Abass.(Picha na Ikulu)
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akizindua Mfumo wa upokeaji wa taarifa sahihi za Udhalilishaji,wakati wa ufunguzi wa Kongamano la Harakati za Kutokomeza Vitendo vya Udhalilishaji Zanzibar, lililoandaliwa na Jumuiya ya Wanasheria Wanawake Zanzibar.(ZAFELA) lililofanyika katika ukumbi wa Sheikh nIdrisa Abdulwakil Kikwajuni Jijini Zanzibar.(Picha na Ikulu)

NA MWANDISHI MAALUM, UNGUJA.

Rais Wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi  amesema umefika wakati wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kuunda tume ya kupambana na Udhalilishaji wa Kijinsia visiwani Zanzibar kwa ajili ya kupambana na udhalilishaji visiwani humo.

Rais Dk. Mwinyi ameyasema hayo kwenye  kongamano la udhalilishaji liloandaliwa na Jumuiya ya Wanasheria Wanawake wa Zanzibar katika ukumbi wa Shekh Idriss Abdul - Wakil, Kikwajuni Jijini Zanzibar.
 Aidha Mhe. Rais Mwinyi amewataka watendaji wa Taasisi zote zinazohusika na suala la udhalilishaji kujipima juu ya utendaji wao. Hii ni baada ya kuendelea kutolewa malalamiko Kwa baadhi ya watu ambao wanashutumiwa Kwa vitendo vya udhalilishaji kuachiliwa huru.
Udhalilishaji sio suala la ubakaji tu, kwani waathirika wakubwa japo wanaonekana ni wanawake lakini wapo wanaume wengi ambao wanadhalilishwa pia. Alisema Mhe. Rais Mwinyi.
“Nimekuja hapa kuwapeni Uhakika wa kwamba ninayo dhamira ya dhati kulimaliza tatizo la udhalilishaji visiwani kwetu. “
Katika hatua nyingine, Mhe. Rais amemtaka Jaji Mkuu wa Zanzibar, Mhe. Omary Makungu kuwahimiza majaji na mahakimu waliochini ya Mhimili wake kutekeleza wajibu wao Kwa wakati na Kwa Uadilifu ili kulinda haki za watu ambao wametendewa unyanyasaji wa kijinsia.
Mhe.  Rais, Dk. Mwinyi, amezishukuru taasisi na asasi binafsi ambazo zimekuwa zikitoa misaada ya kisheria kwa Wananchi wa Zanzibar kwani licha ya Kwamba ni wajibu wa Serikali kutoa huduma na misaada ya kisheria, lakini taasisi hizi zimekuwa msaada mkubwa.

Comments

Popular posts from this blog

CV YA KOCHA MPYA WA SIMBA PABLO FRANCO MARTIN "USIPIME"