RC KUNENGE APOKEA MISAADA YA VIFAA KWA AJILI YA WANAFUNZI WALIOATHIRIKA KUTOKANA NA BWENI LA WASICHANA SEKONDARI YA KIWANGWA KUTEKETEA KWA MOTO
NA
MWANDISHI WETU
MKUU
wa Mkoa wa Pwani Mhe. Abubakar Kunenge amepokea misaada ya vifaa mbalimbali
kuwasaidia wanafunzi waliathirika kutokana na ajali ya moto iliyotokea katika bweni
la wasichana shule ya sekondari Kiwangwa iliyoko jimbo la Chalinze Mkoani Pwani
majira ya saa 1 usiku Julai 22/2021.
“Tumekuja
hapa na wadau ambao wametupatia misada mbalimbali, Jukumu letu la kwanza lilikuwa
ni kuhakikisha watoto wetu wako salama, na kwakweli wako salama na tunamshukuru
mwenyezimungu hatukuweza kupata madhara ya kuweza kupoteza maisha ukiacha
mshtuko walioupata baadhi yao, na jukumu letu la pili ni kuhakikisha kuhakikisha
baada ya kuwa salama wanaendelea kupata sehemu ya makazi ili waendelee na
masomo.” Alisema RC Kunenge.
Alisema
vifaa vya msingi kama magodoro, mashuka, mito, madaftari, na mahitaji mengine
ya watoto hao wa kike vimepatikana.
Alisema
katika ajali hiyo mabweni mawili ya wasichana yaliteketea kwa moto, na
amewashukuru sana wadau hao kutokana na misaada hiyo ambayo katika wakati huu
watoto hao wanaweza kuendelea na masomo.
“Bado
tunaendelea kupokea misada, tumeelekeza Halmashauri iwe imejenga walau bweni
moja ndani ya mwezi mmoja na kuna wabia wengine wametuahidi kujenga bweni la
pili, na kwakweli hii ndiyo Tanzania tunayoifahamu tunapokuwa na changamoto
tunakuwa kitu kimoja na tunasaidiana.” Alifafanua.
Alisema
kutokana na ajali hiyo ambayo sasa ni mara ya pili kutokea, Mkoa umeunda timu
kuchunguza chanzo cha moto huo ni nini.
“Tuna
historia katika shule hii……, hii ni mara ya pili bweni la watoto wa kike
linaungua hivyo tunataka tujue, chanzo ni upande wa ujenzi kwa maana ya
utaalamu, au kuna matumizi kwa wale wanaotumia mabweni hayo au labda ni hujuma,”
alifafanua.
Alisema
mabweni ya sasa yatajengwa kwa kuzingatia utaratibu wa sasa na kuzingatia
taratibu za kiusalama kulingana na maelekezo ya TAMISEMI.
“Kubwa
ni kwamba watoto wateendelea na masomo, wako kwenye mikono salama kwani urithi
mkubwa kwa watoto wetu ni kuwapatia elimu. Na niendelee kumshukuru Mhe. Rais
Samia Suluhu Hassan kwa upendo wake kwani metupa pole kutokana na ajali hii.”
Alisema.
Pia
amempongeza Rais mstaafu wa awamu ya nne Mhe. Dkt. Jakaya Kikwete kwa moyo wake
wa upendo, kwa kutembelea eneo hilo la ajali nay eye ndiye aliyeanzisha shule
hiyo wakati huo akiwa mbunge.
Kwa
upande wake, Mbunge wa jimbo la Chalinze, Mhe., Ridhiwani Kiwkete alisema yeye
kama mbunge anawahakikishia wanafunzin hao wanarudi kwenye hali yao ya kawaida.
“Nikuhakikishie
Mkuu wa Mkoa, mahitaji kuhusiana na wanafunzi yatakayowawezesha kuendelea kusoma
yanapatikana.” Alisema
Alimpongeza
Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhe. Abubakar Kunenge kwa kuonyesha uongozi kufuatia
ajali hiyo.
“Leo
ni siku ya kupata uongozi na faraja kutoka kwako na wafadhili wetu waliokuja, tunaamini
katika uongozi wako na wewe umetuonyesha uongozi katika kipindi cha matatizo,
walionifundisha siasa na uongozi waliniambia kiongozi mzuri anaonekana katika
kipindi cha shida na siyo kipindi cha raha na wewe umekuwa mfano bora wa kuigwa
na sisi tunaendelea kujifunza kutoka kwako,…haujatuacha siku ya kwanza
tulipotokewa na janga hili na umeendelea kuwa nasi leo tunapopokea mahitaji
haya.” Alisifu na kuongeza…………………Hakika naiona nguvu yako Mhe. Mkuu wa Mkoa.
Aidha
kwa upande Ali Yusuf Abdulrahman Surya, mwenyekiti taasisi ya Miraj-Tanzania,
alisema binadamu ana mahitaji mawili ya kiroho na kimwili.
Mahitaji
ya kirohoro tunawapatia maneno ya mwenyezimungu ili roho ipate dawa, itulie
ifanye ibada na kufanya mwili mwema, na pia kuna mahitaji ya mwili, makazi,
mavazi, vyakula na vinginevyo.
“Ombi
la Mkuu wa Mkoa la kupata mabweni mawili Inshaallah tunawaahidin kuwa tutajenga.”
Aliwahakikishia.
Comments
Post a Comment