COSTECH YAWAALIKA WANANCHI KUTEMBELEA BANDA LAO KATIKA MAONESHO YA SABASABA

Mbunifu kutoka Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) Bw.Yoel Max (kulia) akiwa na mwenzake akionesha moja kadi ambayo inamtambulisha mjasiliamali ambaye atajiunga na programu ya Yu-Sokoni na kutambulika.

*******************

Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) inawakaribisha wananchi kwa ujumla kwenye banda lao katika Maonesho ya 45 ya Biashara ya Kimataifa kwenye viwanja vya Julius Nyerere maarufu Sabasaba jijini Dar es Salaam kujionea teknolojia zilizoibuliwa na Tume hiyo.

Akizungumza katika Maonesho hayo Mmoja wa Wabunifu walioibuliwa na Tume hiyo Bw.Yoel Max amesema uwepo wa COSTECH wameweza kusaidia kuibua wataalamu wengi na wabunifu ambao wengi wameweza kujiajiri na kuajiriwa kwenye makampuni makubwa hapa nchini kupitia Teknolojia.

Bw.Max ambaye ameweza kubuni programu maalumu ambayo inasaidia kuagiza ama kuuza bidhaa mtandaoni kwa usalama na uhakika na kuweza kuwanufaisha wajasiliamali wengi ambao wanatumia programu hiyo inaiyoitwa Yu-Sokoni.

"Kumekuwa na matapeli wengi mtandaoni, wamekuwa wakitangaza bidhaa kwenye mitandao na wengi hutuma fedha zao na kuweza kutapeliwa.Hii imesababisha mpaka wale ambao ni waaminifu kuonekana na wao ni matepeli". Amesema Bw.Max.

Amesema Yu-Sokoni inapatikana Google Playstore na ni rahisi kujisajili kitu muhimu ni smartphone yako au kompyuta mpakato pamoja na namba ya NIDA kwaajili ya kufahamu taarifa zako zaidi.

Pamoja na hayo ameishukuru COSTECH kwasababu mpaka walipofikia hapo juhudi kubwa zimefanywa na Tume hiyo toka kutengeneza wazo na njia za kufanya ili kufanikisha jambo.

"Kwa wale ambao wanakuwa wanaanza biashara changamoto huwa ni kubwa hasa uelewa wa sheria yaani ufanye nini uende wapi ili usitoke nje ya sheria kwahiyo COSTECH imeweza kusaidia kwa kiasi kikubwa mpaka zoezi hili limekamilika". Amesema Bw.Max.

Comments

Popular posts from this blog

CV YA KOCHA MPYA WA SIMBA PABLO FRANCO MARTIN "USIPIME"