WAJUMBE WA KIKAO CHA MASHIRIKIANO KATI YA SMZ NA SMT WAKAGUA MIRADI YA SEKTA YA UJENZI

Meneja wa Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS), mkoa wa Tanga, Mhandisi  Alfred Ndumbaro, akitoa Taarifa ya mradi wa mizani ya Pongwe  na Barabara ya Tanga – Pangani (Km 50),  kwa wajumbe wa kikao cha mashirikiano kati ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (SMT), walipokuwa wakikagua miradi hiyo, mkoani Tanga. 

Muonekano wa Gari la mizigo likipima uzito katika kituo cha mizani cha Pongwe, mkoani Tanga.

Kiongozi wa zamu katika Kituo cha mizani cha Pongwe, mkoani Tanga, Elias Magugudi, akielezea namna huduma za upimaji uzito wa magari zinavyofanyika katika kituo hicho wakati wajumbe wa kikao cha mashirikiano kati ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, walipofika hapo kujionea utendaji wa mizani hiyo.

Abiria wakiingia katika kivuko cha MV Pangani II kwa ajili ya kuvuka kuelekea upande wa Bweni, Tanga. Kivuko hicho chenye uwezo wa kubeba abiria 100 na magari Sita sawa na tani 50, kinatoa huduma ya usafirishaji kati ya Pangani na Bweni, mkoani Tanga.

Muonekano wa nyumba ya makazi ya Jaji ambayo imejengwa na Wakala wa Majengo Tanzania (TBA), mkoa wa Tanga. Wajumbe wa kikao cha mashirikiano kati ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  walifika hapo kujionea utekelezaji wa mradi huo.(PICHA NA WUU)

Comments

Popular posts from this blog

CV YA KOCHA MPYA WA SIMBA PABLO FRANCO MARTIN "USIPIME"