Wednesday, June 16, 2021

UJENZI WA MELI MPYA YA MV MWANZA WAFIKIA 74%

Kazi mbalimbali za ujenzi wa Meli mpya ya MV. Mwanza Hapa Kazi Tu ukiendelea kwa kasi kubwa katika Bandari ya Mwanza Kusini. Ujenzi wa Meli hiyo umefikia asilimia 74% na unatarajiwa kukamilika mapema mwakani.

Meli hii itakuwa na uwezo wa kubeba abiria 1200 pamoja na mizigo tani 400, na inatarajiwa kufanya safari za kutoka Mwanza-Bukoba, Musoma na nchini Uganda. Hapo jana Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan alitembelea kukagua ujenzi wa Meli hiyo mkoani Mwanza. 0 comments:

Post a Comment