RC SHIGELA AFUNGUA MAFUNZO YA TAHMINI ZA ULEMAVU ULIOTOKANA NA AJALI NA MAGONJWA YATOKANAYO NA KAZI KWA MADAKTARI WA KANDA YA MASHARIKI YANAYORATIBIWA NA WCF
NA
MWANDISHI WETU, MOROGORO
MKUU
wa Mkoa wa Morogoro Mhe. Martine Shigela amewaasa madaktari wanaohudhuria
mafunzo ya kuwajengea uwezo wa kufanya tathmini za ulemavu uliotokana na ajali
na magonjwa yatokanayo na kazi kwa watumishi wa sekta ya Umma na Binafsi
kufanya kazi hiyo kwa wepesi kwa weledi na kwa wakati ili wahusika waweze kupata
fidia stahiki kama inavyopasa.
Mhe.
Shigela ameyasema hayo Jumatatu Juni 14, 2021 mjini Morogoro wakati
akifungua mafunzo hayo yaliyoandaliwa na Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF)
na kuwaleta pamoja madaktari na watoa huduma za afya 100 kutoka mikoa ya Mtwara,
Lindi, Dar es Salaam, Pwani na Morogoro.
“Kufanya
tathmini kunahitaji utaalamu, uelewa, ujuzi wa namna nzuri zaidi ya kufanya
tathmini ili kuondoa malalamiko kwa anayefanyiwa tathmini, Tathmini ya mtu
aliyelemaa si sawa na kufanya tathmini ya majengo, vyombo au mshine, tathmin ya
binadamu ina changamoto na ndio maana WCF imeteua baadhi ya wataalamu ili kuja
kupata mafunzo haya.” Alibainisha.
Alisema
mafunzo hayo yataweza kujenga uwezo kwa wataalamu wengi hadi ngazi ya wilaya na
hivyo kuwafikia watu wengi kwa wakati.
Aliusifu
Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi kwa kufanya kazi nzuri ambapo Serikali
inayoongozwa na Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan, kupitia WCF imechangia kwa
kiwango kikubwa kuwalipa watu wenye ulemavu uliotokana na ajali katika utumishi
wao mahala pa kazi na hivyo umeweza kuzifanya familia ziweze kuendelea na
maisha kama zilivyokuwa wakati mama au baba alivyokuwa na uwezo wa kawaida wa kuzalisha.
Lakini pia alitoa angalizo kwa waajiri kuhakikisha wanajisajili na Mfuko, kutoa taarifa sahihi za wafanyakazi na kutoa michango kwa wakati ili wafanyakazi waweze kunufaika endapo watapata matatizo wakat wakitekeleza majukumu yao ya kikazi.
Akimkaribisha
Mkuu wa Mkoa kufungua mafunzo hayo, Mkurugenzi Mkuu wa WCF Dkt. John Mduma
alisema mafunzo hayo ya siku tano ni kama sehemu ya hatua muhimu kuuwezesha
Mfuko kutekeleza vema jukumu la kufanya tathmini sahihi na kwa wakati pindi
mfanyakazi anapoumia au kuugua kutokana na kazi,
“Mafunzo
haya ni moja ya mikakati ya kuondoa changamoto ya kuwafikia walengwa kwa muda
na kwa haraka na hivyo kutoa tathmini kwa wakati.” Alisema Dkt. Mduma.
Alisema
wawezeshaji wa mafunzo hayo ni wataalamu wabobezi ambao wamekuwa wakishirikiana
na Mfuko kuandaa miongozo ya tathmini ya ulemavu.
Aliwashukuru
wataalamu (Wawezeshaji) na taasisi ambazo zimewaruhusu ili kushirikiana na
Mfuko ambapo alizitaja kuwa ni pamoja na Hospitali ya Taifa Muhimbili,
Hospitali ya Saratano ya Ocean Road, Hospitali ya Mifupa Muhimbili Chuo Kikuu
Cha Sayansi Shirikishi MUHAS na Wakala
wa Usalama na Afya Mahala pa Kazi OSHA.
“Mfuko
unatambua umuhimu wa mafunzo haya kwa watalamu na ndio maana yamepangwa kuwa
endelevu na yamekuwa yakifanyika tangu Mfuko ulipoanza kutekeleza majukumu
yake.” Alisema Dkt. Mduma.
Happy being part of the training. It has been a very useful one to our setting as medical practitioners
ReplyDelete