RAIS DKT. MWINYI AKUTANA NA UONGOZI WA ZSSF

 RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi ameutaka uongozi wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii Zanzibar (ZSSF) kutambua kwamba madhumuni ya mfuko huo ni kuwasadia wastaafu ili waweze kuishi vizuri baada ya ustaafu wao.

 

Rais Dk. Mwinyi ameyasema hayo leo Ikulu jijini Zanzibar wakati alipokutana na kufanya mazungumzo na Uongozi wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii Zanzibar (ZSSF) ukiongozwa na Mkurugenzi Mwendeshaji wa Mfuko huo Nassor Shaaban Ameir.

 

Katika maelezo yake alisema kwamba kuna utofauti mkubwa wa wastaafu wa hapa nchini na nchi nyengine duniani ambapo kwa upande wa nchi hizo wastaafu baada ya kustaafu kazi ndipo huishi vizuri zaidi kuliko wakiwa kazini.

 

Rais Dk. Mwinyi alisema kuwa watu wamekuwa wakitoa fedha zao na kuziweka katika Mfuko wa ZSSF katika kipindi  chao chote cha kazi ambapo fedha hizo zimekuwa zikiekezwa kwa miaka mingi hivyo, wamekuwa na matarajio makubwa kwamba watapata faida kubwa baada ya kustaafu lakini kinachotoka ni tofauti.

 

Alisema kwamba moja ya dhamana kubwa uliopewa Mfuko huo wa ZSSF ni kuhakikisha unawekeza vizuri na unatapa faida nzuri ili kuhakikisha wastaafu wanaishi vizuri na sio kupigiwa hesabu kwa Walichochangia wakati wako kazini.

 

Rais Dk. Mwinyi alieleza kwamba mstaafu wakati yuko kazini amekuwa akichangia hadi anafika muda wa kustaafu wa miaka 60 anakuwa tayari ameshatengeneza faida na kueleza kwamba hakuna sababu ya mstaafu kutopata maslahi mazuri.



Comments

Popular posts from this blog

CV YA KOCHA MPYA WA SIMBA PABLO FRANCO MARTIN "USIPIME"