MHE. BASHUNGWA: KAZI INAENDELEA KUENEZA KISWAHILI DUNIANI

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Innocent Bashungwa ameendelea kutekeleza agizo la Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan la kukuza Kiswahili baada ya leo Aprili 16, 2021 kuikabidhi Taasisi ya British Council, Kamusi ya Kiswahili.

Mhe. Bashungwa ambaye alikuwa Mgeni Rasmi katika warsha ya Namna Kijana Anavyoweza Kutumia Ubunifu Kujiendeleza Kiuchumi iliyoandaliwa na British Council, ametumia fursa hiyo kukinadi Kiswahili kwa kumkabidhi Mkurugenzi wa Taasisi hiyo zawadi ya Kamusi kama sehemu ya juhudi za kuongeza soko na matumizi ya lugha hiyo. 

“Moja ya maagizo aliyoyatoa Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan kwa Wizara yetu kuhusu Kazi Iendelee ni kuongeza jitihada na maarifa katika kukua kwa soko na utumiaji wa lugha ya Kiswahili nje ya mipaka ya Tanzania,” ameeleza Mhe. Bashungwa.

Waziri Bashungwa amesema kuwa kueneza Kiswahili  ni njia  na namna mojawapo ya kumuezi aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Hayati Dkt. John Pombe Magufuli ambaye alikuwa bingwa wa kunadi lugha hiyo adhimu.



 

Comments

Popular posts from this blog

CV YA KOCHA MPYA WA SIMBA PABLO FRANCO MARTIN "USIPIME"