RAIS SAMIA AMTEUA DKT. PHILIP ISIDOR MPANGO KUWA MAKAMU WA RAIS WA TANZANIA

 RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan amemteua Dkt. Philip Mpango (pichani) kuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, SPIKA wa Bunge Mhe. Job Ndugai ameliambia Bunge jijini Dodoma leo Machi 30, 2021.

Dkt. Mpango alikuwa WAZIRI wa Fedha na Mipango na Mbunge wa Jimbo la Buhigwe mkoani Kigoma.

Bunge linatarajiwa kumpitisha KATIKA kikao kinachoendelea kwa kumpigia kura ambapo inatakiwa wabunge ASILIMIA 50 wamuunge mkono. Wabunge 363 wamepiga kura na hakuna kura iliyoharibika na hakuna kura ya hapana hata moja. Kwahiyo amepata ASILIMIA 100 ya kura zote.



Comments

Popular posts from this blog

CV YA KOCHA MPYA WA SIMBA PABLO FRANCO MARTIN "USIPIME"