TANZANIA INAZIADA YA UMEME MEGAWATI 424.28
NA
K-VIS BLOG, MOROGORO
TANZANIA
kwa sasa inazalisha umeme Megawati 1, 604.81 kwa siku na mahitaji ya juu kabisa ya
umeme nchi nzima ni Megawati 1,180.53, na hivyo kufanya kuwepo kwa ziada ya umeme Megawati 424.28, Meneja Mwandamizi wa Uzalishaji Umeme (power
generation) kutoka Shirika la Umeme Nchini TANESCO, Mhandisi Stephen Manda (pichani juu) amesema.
Akiwasilisha
mada kuhusu moja ya jukumu la TANESCO la kuzalisha umeme (Generation) kwenye
kikao kazi cha TANESCO na Wahariri Waandamizi wa vyombo vya habari leo Februari
26, 2021 kwenye ukumbi wa NSSSF mkoani Morogoro alisema TANESCO inazalisha
Megawati 1,393.45 na wazalishaji binafsi wanachangia kiasi cha Megawati 211.36.
Akifafanua
zaidi, Mhandisi Manda alisema Gridi ya Taifa inabeba umeme Megawati 1,567.951 ambapo
asilimia 87 ya umeme huo unazalishwa na TANESCO huku asilimia 33.126 unatoka
kwa wazalishaji binafsi.
Mhandisi
Manda alisema, ni matatrajio ya taifa kuwa mradi mkubwa wa umeme wa Julius
Nyerere wa Megawati 2115 utaleta ongezeko kubwa la umeme na hivyo kuleta nafuu
kubwa ya gharama za umeme na hivyo pato la taifa na wananchi kwa ujumla. Aidha alisema kwa sasa umeme wa Gesi ndio unaongoza kwa kuchangia kiasi kikubwa cha umeme kwa asilimia 56, huku umeme wa maji ukichangia asilimia 36, mafuta asilimia 7 umeme utokanao na taka asilimia 1.
Comments
Post a Comment