TANESCO YAJA NA MFUMO "MTEJA UKINUNUA UMEME HULAZIMIKI KUINGIZA TOKEN KWENYE MITA, UNAINGIA WENYEWE MOJA KWA MOJA BAADA YA MALIPO"
SHIRIKA
la Umeme nchini TANESCO linatarajia kuweka mfumo utakaomuwezesha mteja
aliyenunua umeme kupitia simu ya kiganjani kutolazimika kuingiza namba (TOKEN)
kwenye mita na badala yake umeme utaingia moja kwa moja kwenye mita mara tu baada ya kukamilisha malipo.
Meneja
Mwandamizi Usambazaji Umeme Mhandisi Athanasius Nangali(pichani juu) amewaambia Wahariri wa vyombo vya
habari wanaoshiriki kikao kazi baina ya TANESCO na Wahariri mjini Morogoro Februari
26, 2021.
“TANESCO
tunaendelea kuboresha zaidi utoaji wa huduma zetu na sasa hivi tuko kwenye
mpango wa kuweka mfumo ambapo mteja atakaponunua umeme kwenye simu yake au
kwingineko basi umeme utaingia moja kwa moja kwenye mita yake nyumbani na hatalazimika
tena kuingiza namba (TOKEN) kwenye mita.” Mhandisi Nangali amefafanua.
Akifafanua
zaidi alisema TANESCO tayari imemuajiri mtaalamu mshauri kutoka serikalini ili
akague specification na akishamaliza kuzikagua tunaingia kwenye huo mfumo moja
kwa moja.
“Lengo
letu sisi tunataka wateja wetu wapate huduma ya umeme bila matatizo yoyote”.
Alifafanua.
Comments
Post a Comment