Tuesday, February 23, 2021

STAMICO YAPATA TUZO YA MCHANGIAJI BORA WA GAWIO SERIKALINI.

 

Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) imepata tuzo ya uchangiaji bora wa Gawio Serikalini  katika sekta ya madini. Tuzo hii imetolewa na Wizara ya Madini katika mkutano unaondelea katikajijini DsM.

Akiongea mara baada ya kupokea tuzo hiyo Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa STAMICO Dkt Venance Mwasse amesema amefurahi kupata tuzo hiyo kwa kuwa ni sehemu ya kutambua na kuthamini michango wa Shirika kwa niaba wa Watanzania.

Amesema STAMICO itaendelea kutoa Gawio Serikalini kwa kuwa Shirika limejizatiti katika kuhakikisha sekta ya madini inawanufaishana  Watanzania wote.

0 comments:

Post a Comment