Friday, February 26, 2021

RAIS DKT. MWINYI AJUMUIKA NA WAUMINI WA KIISLAM KATIKA SALA YA IJUMAA ILIOFANYIKA MASJID RAUDHA DARAJA BOVU

 

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhajj Dk. Hussein Ali Mwinyi akisalimiana na Wananchi alipowasili katika viwanja vya Masjid Raudha Daraja bovu Wilaya ya Magharibi “A” Unguja kuhudhuria Ibada ya Sala ya Ijumaa iliofanyika katika msikiti huo leo 26-2-2021.

IMAMU wa Masjid Raudha Daraja Bovu Wilaya ya Magharibi “A” Unguja Sheikh. Ali Faki Abdalla akizungumza na kutowa neno la shukrani kwa niaba ya Wananchi na Waumini wa Kiislam kwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhajj Dk. Hussein Ali Mwinyi kwa kufanikisha kuwamalizia ujenzi wa Masjid yao, shukrani hiyo imetolewa baada ya kumalizika kwa Sala ya Ijumaa iliofanyika leo.26-2-2021 katika msikiti huo.

 

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhajj Dk. Hussein Ali Mwinyi, akizungumza na Waumini wa Kiislam wa Masjid Raudha Daraja Bovu Wilaya ya Magharibi “A” Unguja, baada ya kumalizika kwa Sala ya Ijumaa, iliofanyika katika Masjid hiyo leo 26-2-2021, na kupokea shukrani zao.

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhajj Dk. Hussein Ali Mwinyi akitikia dua ikisomwa na Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh Saleh Omar Kabi baada ya kumalizika kwa Sala ya Ijumaa iliofanyika katika Masjid Raudha Daraja Bovu Wilaya ya Magharibi “A” Unguja.

 

WAUMINI wa Dini ya Kiislam wakiitikia dua ikisomwa na Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh Saleh Omar Kabi.(hayupo pichani) baada ya kumalizika kwa Sala ya Ijumaa iliofanyika katika Masjid Raudha Daraja Bovu Wilaya ya Magharibi “A” Unguja

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhajj Dk. Hussein Ali Mwinyi akiwasalimia Wananchi wakati akitoka katika Masjid Raudha Daraja Bovu Wilaya ya Magharibi “A” Unguja baada ya kumalizika kwa Sala ya Ijumaa iliofanyika leo katika msikiti huo.(Picha na Ikulu)

0 comments:

Post a Comment