RC KUNENGE KUKUTANA NA WAFANYABIASHARA NA WAWEKEZAJI DAR DISEMBA 10.


Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Aboubakar Kunenge (pichani juu) anatarajia kukutana na Wafanyabiashara na Wawekezaji Jijini humo mnamo Disemba 10 Mwaka huu kwenye ukumbi wa mikutano wa Mwalimu Nyerere posta.

RC Kunenge amesema lengo la mkutano huo ni kuweka mazingira Bora ya Uwekezaji na biashara ili kila mmoja aweze kunufaika na shughuli anayoifanya.

Aidha RC Kunenge amesema kupitia mazingira Bora ya Biashara na Uwekezaji itarahisisha ukusanyaji mzuri wa Kodi na ongezeko la ajira kwa wananchi.

Comments

Popular posts from this blog

CV YA KOCHA MPYA WA SIMBA PABLO FRANCO MARTIN "USIPIME"