11/26/2020

KIFO CHA DIEGO MARADONA: SERIKALI YATANGAZA SIKU TATU ZA MABOLEZO

 Argentina imetangaza siku tatu za maombolezo ya kitaifa kufuatia kifo cha gwiji wa kusakata kabumbu Duniani, Diego Armando Maradona aliyefariki Novemba 25, 2020 akiwa na umri wa miaka 60.

Taarifa ya ofisi ya Rais wa nchi hiyo imesema, Rais ametangaza kuwa maombolezo hayo yameanza siku mwanasoka hiyo alipofariki siku ya Jumatano.

Maradona amefariki dunia kutokana na mshtuko wa moyo ikiwa ni siku chache baada ya kufanyiwa operesheni ya kuondoa uvimbe kichwani.

Mwanasoka hiyo wa zamani alijizolea umaarufu mkubwa mnamo mwaka 1986 wakati huo akiichezea timu ya Taifa ya Argentina na kutwaa kombe hilo.



    

0 comments:

Post a Comment