HUDUMA YA MAJI NI NYENZO YA MSINGI KATIKA KUONDOSHA UMASIKINI

Katibu Mkuu, Wizara ya Maji Mhandisi Anthony Sanga akiongea na wajumbe wa Bodi za Wakurugenzi wa Mamlaka za Majisafi na Usafi wa Mazingira (hawapo pichani) zipatazo 15 kutoka mikoa ya Nyanda za Juu Kusini katika kikao kazi alichowataka wajumbe wa bodi hizo kusimamia mamlaka za maji ili kufikia lengo la Serikali la kumfikishia kila mwananchi huduma ya maji. 
Sehemu ya washiriki wa kikao kazi kilichowakutanisha wajumbe wa Bodi za Wakurugenzi wa mamlaka za majisafi na usafi wa mazingira, wakimsikiliza Katibu Mkuu, Wizara ya Maji Mhandisi Anthony Sanga (hayupo pichani). Bodi hizo zinajukumu la kusimamia mamlaka za maji.
Mkurugenzi Msaidizi-Huduma na Ufuatiliaji Mhandisi Lyidia Joseph akiwasilisha mada kuhusu Uongozi na Menejimenti kwa wajumbe wa bodi za Wakurugenzi kutoka Mamlaka za Maji 15 za mikoa ya Nyanda za Juu kusini, katika ukumbi wa Halmashauri ya Mji wa Njombe.
 TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
 
HUDUMA YA MAJI NI NYENZO YA MSINGI KATIKA KUONDOSHA UMASIKINI

Upatikanaji wa majisafi, salama na yenye kutosheleza ni nyenzo muhimu katika kuongeza ubora wa maisha, kupunguza makali ya athari zinazotokana na umaskini na kuongeza kipato cha wananchi. 
Katibu Mkuu, Wizara ya Maji Mhandisi Anthony Sanga amesema hayo wakati wa kikao kazi cha  Bodi za Wakurugenzi kinachofanyika mjini Njombe na kuhusisha bodi za Wakurugenzi kutoka mamlaka 15 zinazotoa huduma ya majisafi kwa wananchi.

Mhandisi Sanga, katika kikao hicho, amesema tafiti za afya zinaonesha kuwa upatikanaji wa majisafi na salama hupunguza zaidi ya asilimia hamsini ya magonjwa ya kuambukiza yatokanayo na maji yasiyo salama, na kusisitiza kuwa kwa kutambua umuhimu huo wa maji kwa afya na maendeleo ya wananchi, lengo la Serikali ni kuwafikishia wananchi wote huduma ya majisafi na salama kwa asilimia 100.

Kuhusu Bodi za Wakurugenzi, ameongeza kuwa moja ya majukumu ya bodi hizo ni kushughulikia malalamiko ya Watumishi na wateja wa mamlaka za maji kwa wakati na kuhakikisha mamlaka zinakuwa na mipango ya kupanua utoaji wa huduma katika maeneo yake na kuwakumbusha wajumbe wa bodi kuwa wamepewa dhamana kubwa na Waziri wa Maji aliyewateuwa ili kufanikisha kazi ya kufikisha huduma ya maji kwa wananchi wote.

Mamlaka za Majisafi na Usafi wa Mazingira zinazoshiriki kikao kazi ni Mamlaka ya Mbeya, Iringa, Tabora, Njombe, Sumbawanga, Kigoma, Mtwara, Makambako, Wanging’ombe, Mafinga, Tukuyu, MANAWASA, Makonde, Chunya na Kyela Kasumulu.
Mamlaka za Majisafi na Usafi wa Mazingira ni Taasisi za Serikali zinazojitegemea ambazo zilianzishwa mwaka  1997 kupitia akaunti maalum chini ya Sheria ya Mwaka 1961 (Cap Ordiance 281 Misceleneous Ammendment ACT). Baadae ilitungwa Sheria Na. 12 ya Maji  na Usafi wa Mazingira ya mwaka 2009 ambayo ilzitambua mamlaka. Hivi sasa mamlaka ipo Sheria Namba  5  ya Maji na Usafi wa Mazingira ya mwaka 2019 ambayo pamoja na mengine imezitambua mamlaka na kuboresha masuala mbalimbali kuziongezea ufanisi katika kutoa huduma ya majisafi kwa Watanzania.


Comments

Popular posts from this blog

CV YA KOCHA MPYA WA SIMBA PABLO FRANCO MARTIN "USIPIME"