RAIS MAGUFULI ATOA MKONO WA POLE KWA FAMILIA YA MWANACHAMA WA CCM MAREHEMU BRITON WILFRED HUKO TUNDUMA



Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Mama Mzazi wa Marehemu Briton Wilfred Mollel, Roda Bryson Mwaisongole Tunduma mkoani Songwe. 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa amewashika mkono Watoto wawili wa aliyekuwa Mwanachama wa CCM Marehemu Briton Wilfred Mollel Tunduma mkoani Songwe leo tarehe 02 Oktoba 2020. PICHA NA IKULU



 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akisali pamoja na Familia ya Marehemu Briton Wilfred Mollel, kulia ni Mama Mzazi wa Marehemu Roda Bryson Mwaisongole, mke wa Marehemu Salome Philemon Mayao pamoja na Watoto wake wawili. Marehemu Briton aliuwawa tarehe 25 Agosti, 2020 Tunduma mkoani Songwe na ameacha Watoto watatu. Marehemu Briton alikuwa Mkuu wa Mafunzo na Mkuu wa Itifaki UVCCM Wilaya Momba
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akimkabidhi rambirambi yake ya Sh. Milioni 3 Mama Mzazi wa Marehemu Briton Wilfred Mollel, Roda Bryson Mwaisongole Tunduma mkoani Songwe ili ziwasaidie katika kipindi hiki kigumu.

Comments

Popular posts from this blog

CV YA KOCHA MPYA WA SIMBA PABLO FRANCO MARTIN "USIPIME"