Tuesday, September 22, 2020

RC KUNENGE AKUTANA NA WALIMU DAR, AWAHAKIKISHIA KUWA SERIKALI ITAENDELEA KULIPA MALIMBIKIZO YOTE WANAYODA

NA MWANDISHI WETU.

Mkuu Wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Aboubakar Kunenge leo amefanya kikao kazi na mamia ya walimu wa Shule za Msingi zilizopo Wilaya ya Ilala kwa lengo la kujadili changamoto zinazowakabili na kuangalia namna bora ya kuendelea kuboresha hali ya elimu ambapo amewahakikishia Walimu kuwa Serikali inaendelea kulipa malimbikizo yote wanayodai.

RC Kunenge amesema baada ya Kikao na walimu wa Ilala pia amepanga kukutana na Walimu Wa Wilaya nyingine za Mkoa huo ili aweze kuzipati majibu changamoto zinazowakabili ambapo amewapongeza walimu wote Wa Mkoa huo kwa kazi nzuri wanayoifanya jambo linalofanya mkoa huo kuwa kinara Wa ufaulu kila mara.

Aidha RC Kunenge amemuelekeza Mkurugenzi Wa Manispaa ya Ilala kuhakikisha anatoa kipaombele cha ajira kwa walimu ili kuweza kukidhi changamoto ya uhaba Wa walimu Kwa baadhi ya shule.

Pamoja na hayo RC Kunege amekemea vikali vitendo vya kuvuja Kwa mitihani kwa baadhi ya shule za sekondari na kuwataka wahusika kuwa makini na jambo hilo ili lisiweze kuchafua sifa nzuri ya Mkoa.

Hata hivyo RC Kunenge ametoa wito Kwa Walimu na wananchi Wa mkoa huo kuhudhuria mikutano ya Kampeni za wagombea mbalimbali ili waweze kuchagua viongozi wenye kuleta maendeleo.

 

0 comments:

Post a Comment