ERB YARIDHISHWA NA UJENZI WA MIRADI YA KIMKAKATI
NA MWANDISHI WETU, MOROGORO
BODI
ya Usajili wa Wahandisi nchini (ERB), imeridhishwa na kazi za ujenzi wa
miundombinu ya kisasa na kimkakati inayojengwa mkoani Morogoro kwa kuwa imezingatia
viwango vya kihandisi, na ubora unaowiana
na thamani ya fedha.
Msajili
wa Wahandisi Eng. Patrick Barozi amesema hayo alipokagua miradi ya kimkakati ya
soko la kisasa la Manispaa ya Morogoro, machinjio ya kisasa ya Nguru Hills
Ranch na miundombinu ya umwagiliaji katika
shamba la miwa la Mbigiri katika kiwanda cha miwa cha Mkulazi.
“Tunawapongeza
wahandisi waliofanyakazi katika miradi hii kwa kuwa wabunifu na kuzingatia
weledi na viapo vyao hali itakayosababisha miradi hii kukamilika kwa wakati na
kutioa fusra za ajira, elimu na biashara kwa wananchi”, amesema Eng. Barozi.
Amesema
ukaguzi wa miradi inayotekelezwa na wahandisi ni sehemu muhimu ya majukumu ya ERB
lakini pia zoezi hilo ni fusra kwa wahandisi waliopo katika mafunzo kujifunza
na kubadilishana uzoefu na changamoto na wahandisi walioko kwenye miradi na
hivyo kuwajengea uwezo wahandisi wapya.
Eng.
Barozi ametoa wito kwa vyuo vikuu nchini kuongeza udahili wa wanafunzi katika
fani zenye upungufu wa wataalam ili kuepuka kutumia fedha nyingi kuajiri
wataalam kutoka nje ya nchi.
Nae
msimamizi wa ujenzi wa soko la Manispaa ya Morogoro Eng. Juma Gwisu amesema ujenzi wa soko hilo
umekamilika kwa asilimia 99 na kazi inayoendelea ni kuwapanga wafanyabiashara
katika maeneo yao.
Zaidi
ya wafanyabiashara elfu mbili wanatarajiwa kunufaika kwa kufanyabiashara katika
soko hilo la kisasa lililogharimu zaidi ya shilingi bilioni 17.
Kwa
upande wake Meneja wa ujenzi wa ranch ya Nguru Hills Eng. Grayson Bambanza
amesema machinjio ya ranch hiyo iko
katika hatua za mwisho za ukarabati mkubwa utakaowezesha kuzalisha nyama
itakayouzwa katika masoko ya kimataifa na hivyo kutoa fursa nyingi za ajira kwa
wataalam wa mifugo na kilimo nchini, kuongeza
biashara ya kununua mifugo na mazao ya shambani toka kwa wakulima na wafugaji na hivyo kukuza uchumi wa
jamii mkoani Morogoro.
“Takriban
ng’ombe mia moja na mbuzi na kondoo mia mbili watakuwa wakichinjwa kila siku katika
ranch hiyo itakapokamilika na asilimia 80 ya nyama kuuzwa nje ya nchi na asilimia
20 pekee ndio itauzwa nchini” amsesisitiza Eng. Bambanza.
Meneja umwagiliaji wa shamba la miwa la Mbigiri katika Kiwanda cha
sukari Mkulazi Eng. Juvenal Matumaini amesema kukamilika kwa mabwawa ya
umwagiliaji katika kiwanda hicho kutawezesha kuanza kwa uzalishaji wa sukari wa
kiwanda hicho kinachotarajiwa kutoa ajira zaidi ya elfu tatu na mia sita
kitakapoanza.
Kiwanda
cha sukari Mkulazi kinachomilikiwa kwa ubia kati ya Mfuko wa Hifadhi ya Jamii
(NSSF), na Jeshi la Magereza kiko katika hatua za mwisho kuanza uzalishaji na
kinatarajiwa kuzalisha tani elfu hamsini za sukari kwa mwaka kitakapoanza kazi
na hivyo kuongeza uzalishaji wa sukari nchini na kutoa fursa nyingi za ajira.
Msajili
wa wahandisi Eng. Patrick Barozi akisisitiza jambo kwa wahandisi
wanaosimamia ukarabati mkubwa wa
machinjio ya kisasa katika ranch ya Nguru Hills Mvomero mkoani Morogoro
Ujenzi
wa mifereji ya kupitisha maji kwenda kwenye mabwawa ya kumwagilia miwa katika
shamba la miwa la Mbigiri ukiendelea, shamba hilo ni sehemu ya mashamba
yanayomilikiwa na kiwanda cha sukari cha Mkulazi mkoani Morogoro.
Msimamizi
wa ujenzi wa soko la Manispaa ya Morogoro Eng. Juma Gwisu
akifafanua jambo kwa wahandisi kutoka Bodi ya Usajili wa Wahandisi (ERB),
walipokagua maenedeleo ya ujenzi wa soko hilo.
Muonekano
wa nje wa soko la kisasa la Manispaa ya Morogoro ambalo ujenzi wake
umekamilika.
Muonekano
wa machinjio ya kisasa katika ranch ya Nguru Hills Mvomero mkoani Morogoro
Comments
Post a Comment