Posts

MRADI WA UBORESHAJI USALAMA WA MILKI ZA ARDHI NZEGA MJINI KUKAMILIKA JUNI 30, 2024

Image
             Na Eleuteri Mangi Utekelezaji wa Mradi wa Uboreshaji Usalama wa Milki za Ardhi (LTIP)katika Halmashauri ya Mji Nzega katika mkoa wa Tabora umetekelezwa kwa asilimia 55 na kutarajiwa   kukamilika Juni 30, 2024. Akimkaribisha Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) Mhe. Japhet Hasunga   na ujumbe wake wakati wa ziara ya Kamati hiyo wilayani Nzega   tarehe 27 Machi 2024, Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Geophrey Pinda amesema utekelezaji wa Mradi wa Uboreshaji Usalama wa Milki za Ardhi katika mji wa Nzega unatekelezwa katika mitaa 14 iliyopo Kata za Nzega Mashariki, Nzega Magharibi, Nzega ndogo, Kitangiri na Uchama. Amebainisha kuwa, katika kata ya Nzega Mjini Mashariki mradi unatekelezwa Mitaa ya Maporomoko, Uwanja wa Ndege, Msoma, Mwaisela, Nyasa pamoja na Kitongo. Aidha, Kata ya Nzega Mjini Magharibi mradi unatekelezwa katika mitaa ya Ipilili, Mbugani, Ushirika na Utemini. Aidha, kwa upande wa Kata ya Nzega

RAIS SAMIA AFUTURISHA MAKUNDI MBALIMBALI JIJINI DODOMA

Image
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimpa futari mtoto yatima Shuraiya Ramadhan (6) wa Kituo cha Watoto Yatima cha Rahman kilichopo Chang’ombe Jijjini Dodoma. Rais Samia aliwaandalia Iftar Viongozi pamoja na Wageni mbalimbali Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma tarehe 27 Machi, 2024. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimpakulia Iftar mtoto Yatima Shuraiya Ramadhan (6) wa Kituo cha Watoto Yatima cha Rahman kilichopo Chang’ombe Jijjini Dodoma. Rais Samia aliwaandalia Iftar Viongozi pamoja na Wageni mbalimbali Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma tarehe 27 Machi, 2024. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiitikia Dua mara baada ya kupata Iftar aliyowaandalia Viongozi pamoja na Makundi mbalimbali Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma tarehe 27 Machi, 2024. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiitikia Dua mara baada ya kupata Iftar aliyowaandalia Viongozi pamoja na Makundi mbalimbali Ikulu Cham

KUTOKA MAGAZETINI LEO MACHI 28, 2024

Image
 

WAZIRI DKT. NCHEMBA AKUTANA NA MKURUGENZI MPYA WA TBL

Image
  Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), akipeana mkono na Mkurugenzi Mtendaji mpya wa Kampuni ya Tanzania Breweries Pls, Bi. Michelle Kilpin, baada ya kufika Ofisi za Hazina (Treasury Square), jijini Dodoma, kujitambulisha, ambapo Mkurugenzi Mtendaji huyo ameipongeza Serikali kwa kuboresha mazingira ya kufanyabiashara na kuahidi kuwa Kampuni yake itaendelea kuchangia maendeleo ya nchi kupitia program mbalimbali za kusaidia jamii na kulipa kodi. Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), kushoto, akisikiliza maelezo ya Mkurugenzi Mtendaji mpya wa Kampuni ya Tanzania Breweries Pls, Bi. Michelle Kilpin (kulia), kuhusu Kampuni yake kuendelea kuchangia maendeleo ya jamii, alipofika kujitambulisha, katika ukumbi wa Mikutano wa Waziri (Treasury Square), jijini Dodoma. Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), akizungumza jambo wakati wa mkutano wake na Mkurugenzi Mtendaji mpya wa Kampuni ya Tanzania Breweries Pls, Bi. Michelle Kilpin (hayupo pichan