Posts

WATAALAMU SEKTA YA MIPANGO MIJI WAKUTANA KUJADILI MAPITIO YA RASIMU YA KANUNI MPYA ZA SHERIA YA MIPANGO MIJI

Image
 Na Eleuteri Mangi, WANMM Wadau wa sekta mipango miji wamekutana Jijini Dodoma kujadili rasimu ya marekebisho ya Kanuni za Sheria za Mipango Miji nchini ili ziendane na mabadiliko ya kasi ya ukuaji miji pamoja mchango wake wa sekta hiyo katika hafua muhimu za kuifadhi mazingira.   Akifungua kikao hicho Januari 30, 2024 jijini Dodoma, Naibu Katibu Wizara ya ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Bi Lucy Kabyemera amesema kuwa ardhi inahitaji kupangwa, kupimwa, kumilikishwa na kuendelezwa ikiwa katika hali nzuri kiuchumi, kijamii na kimazingira. “Natambua ili kufanikisha azma hii, tunahitaji kuwa na kanuni sahihi za kuongoza upangaji wa miji yetu pamoja na matumizi mbalimbali ya ardhi hapa nchini” Naibu Katibu Bi Kabyemera. Upangaji miji unaongozwa na Sheria ya Mipango Miji sura Na. 355 na Kanuni zake za mwaka 2018 ambazo zinahitaji kuboreshwa kutokana na mabadiliko ya kiuchumi, kimazingira, mitazamo ya kimaisha, kimaendeleo pamoja na mitazamo ya kimataifa vimekuwa msingi wa kupitia upya k

TUME YATEUA MADIWANI WANAWAKE WA VITI MAALUM WATANO

Image
Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Mhe. Jaji (R) Jacobs Mwambegele (kushoto) akiongoza kikao cha Tume jijini Dodoma ambapo pamoja na mambo mengine kiliteua madiwani watano (5) wanawake wa viti Maalum. Pamoja nae ni  Katibu wa Tume na Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Bw. Ramadhani Kailima.    Wajumbe wa Tume wakiendelea na  kikao cha Tume jijini Dodoma ambapo pamoja na mambo mengine kiliteua madiwani watano (5) wanawake wa viti Maalum. 

KUTOKA MAGAZETINI LEO JANUARI 30, 2024

Image
 

WAJUMBE TUME YA TAIFA YA UCHAGUZI WATEMBELEA MAONESHO YA WIKI YA SHERIA DODOMA

Image
  Wajumbe wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) wakiongozwa na Makamu Mwenyekiti wa Tume, Mhe. Jaji wa Rufaa (Mstaafu), Mbarouk Salim Mbarouk leo Januari 29,2024 wametembelea maonesho ya maadhimisho ya Wiki ya Sheria kitaifa yanayofanyika katika viwanja vya Nyerere Square Jijini Dodoma. Maonesho ya Wiki ya Sheria yalianza Januari 24, 2024 na yamataraji kufikia tamati Januari 30,2024. Wajumbe wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) wakiongozwa na Makamu Mwenyekiti wa Tume,Mhe. Jaji wa Rufaa (Mstaafu), Mbarouk Salim Mbarouk leo Januari 29,2024 wametembelea maonesho ya maadhimisho ya Wiki ya Sheria kitaifa yanayofanyika katika viwanja vya Nyerere Square Jijini Dodoma. Maonesho ya Wiki ya Sheria yalianza Januari 24, 2024 na yamataraji kufikia tamati Januari 30,2024. Wajumbe wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) wakiongozwa na Makamu Mwenyekiti wa Tume,Mhe. Jaji wa Rufaa (Mstaafu), Mbarouk Salim Mbarouk leo Januari 29,2024 wametembelea maonesho ya maadhimisho ya Wiki ya Sheria kitaifa yanayofanyika ka

KAMISHNA GENERALI WA DAWA ZA KULEVYA AIPONGEZA OFISI YA MKEMIA MKUU WA SERIKALI

Image
    Kamishna Jenerali wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya, Aretas Lyimo (Kulia) akimsikiliza  Mkurugenzi wa Huduma za Sayansi jinai  David Elias k utoka Ofisi ya Mkemia Mkuu wa Serikali aliyekua akimpa maelezo wakati Kamishna huyo alipitembelea Banda la Mkemia Mkuu katika maonesho ya Wiki ya Sheria Kitaifa yanayofanyika katika viwanja vya Nyerere Square Jijini Dodoma.  Kamishna Jenerali wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya, Aretas Lyimo (kushoto) akimsikiliza  Mkurugenzi wa Huduma za Sayansi jinai  David Elias k utoka Ofisi ya Mkemia Mkuu wa Serikali aliyekua akimpa maelezo wakati Kamishna huyo alipitembelea Banda la Mkemia Mkuu katika maonesho ya Wiki ya Sheria Kitaifa yanayofanyika katika viwanja vya Nyerere Square Jijini Dodoma.  Na Sylvester omary, Dodoma Kamishna Jenerali wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya, Aretas Lyimo, ameipongeza Mamlaka ya Maabara ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali kwa utoaji wa haraka wa ripoti za

WAZIRI MAKAMBA AKUTANA NA WAZIRI MKUU WA ITALIA

Image
Waziri Mkuu wa Italia, Mhe. Giorgia Meloni akisalimiana na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. January Makamba (Mb.) katika ukumbi wa mkutano jijini Roma, Italia. Waziri Makamba yupo Roma kumwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan katika Mkutano wa Nne wa Wakuu wa Nchi za Afrika na Italia ulioanza tarehe 28 - 29 Januari 2024 .  

MAWAZIRI WA NISHATI TANZANIA, ZAMBIA WAJADILI UJENZI WA BOMBA JIPYA LA MAFUTA

Image
  *📌Ni la Mafuta Safi kutoka Dar es Salaam hadi Ndola Zambia* *📌Dkt. Biteko asema pia litanufaisha mikoa ya kusini* *📌Zambia yasema ipo tayari kutekeleza mradi huo* *📌Timu ya Wataalam yaanza majadiliano* Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko pamoja na Waziri wa Masuala ya Nishati wa Zambia, Mhe. Peter Kapala leo wamefanya kikao kilicholenga kujadili nia ya Serikali ya Tanzania na Zambia kuanza ujenzi wa bomba la inchi 24 la kusafirisha mafuta safi kutoka Tanzania kwenda Zambia. Kikao hicho kimefanyika tarehe 29 Januari, 2024 jijini Dodoma na kuhudhuriwa na Naibu Waziri wa Nishati, Mhe. Judith Kapinga, Makatibu Wakuu wa Wizara za Nishati, Mhandisi Felchesmi Mramba, (Tanzania) na Dkt. Chisangano Zyambo (Zambia) pamoja na watendaji mbalimbali kutoka Wizara hizo na Mashirika yanayosimamia Mafuta. Dkt. Biteko amesema, majadiliano hayo ya Mawaziri yanatokana na ziara ya Rais wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan aliyoifanya nchini Zambia mwezi Oktoba mwaka 2023 am