WAZIRI MKUU AFUNGA MAFUNZO YA UHAMIAJI, AHIMIZA UADILIFU
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewataka wahitimu 521 wa mafunzo ya Kozi Na. 01/2023 wakatumie vema ujuzi na maarifa waliyoyapata katika kudhibiti vitendo vya uhalifu hususan maeneo ya vipenyo, vituo na mipakani. Ametoa wito huo leo Ijumaa (Septemba 29, 2023) alipofunga mafunzo hayo kwa askari wa Uhamiaji katika Chuo cha Mafunzo ya Uhamiaji cha Raphael Kubaga, Wilayani Mkinga, katika Mkoa wa Tanga. Waziri Mkuu amemshukuru Rais na Amiri Jeshi Mkuu, Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kutekeleza kwa vitendo mpango wake wa kuvijengea uwezo vyombo vya ulinzi na usalama nchini. Mheshimiwa Majaliwa pia amewataka wahitimu hao wakafanye kazi kwa uzalendo, weledi na kutanguliza kwanza maslahi ya Taifa katika kazi zao za kila siku. “Kila mmoja akazingatie maadili na miiko ya kazi na akawe mfano bora wa uadilifu katika kituo atakachopangiwa,” amesisitiza. Aidha, Waziri Mkuu amewataka viongozi wa Jeshi la Uhamiaji wawachukulie hatua kali za kisheria wahitimu ambao watabainika kuwa wanajihusisha na vitend