Posts

KUTOKA MAGAZETINI LEO JUMAMOSI JULAI 29, 2023

Image
 

WAZIRI DKT. NCHEMBA AKUTANA NA MKURUGENZI WA BENKI YA DUNIA KANDA YA AFRIKA

Image
Waziri wa Fedha wa Tanzania, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba Madelu (Mb) (kushoto), akiagana na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Dunia anayesimamia Kundi la Kwanza la Nchi za Afrika (The Executive Director of the World Bank Group – for Africa Group 1 Constituency (AfG1), Dkt. Floribert Ngaruko, baada ya Mkutano wao uliofanyika katika Ukumbi wa Mhe. WF, Ofisi ya Hazina Ndogo, kuhusu ushirikiano kati ya Serikali na Benki hiyo, Jijini Dar es Salaam. Mkutano huo umewashirikisha pia Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, na Mlipaji Mkuu wa Serikali, Dkt. Natu El-maanry Mwamba, Naibu Katibu Bi. Amina Khamis Shaaban, Kamishna wa Idara ya Fedha za Nje, Bw. Rished Bade, Kamishna wa Idara ya Usimamizi wa Deni la Taifa, Bw. Japhet Justine, Kamishna Msaidizi wa Idara ya Fedha za Nje, Bw. Robert Mtengule na maafisa wengine wa Wizara ya Fedha. Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Dunia anayesimamia Kundi la Kwanza la Nchi za Afrika (The Executive Director of the World Bank Group – for Africa Group 1 Constituency (

KWA MARA YA KWANZA MATIBABU YA UZIBUAJI WA MISHIPA YA DAMU YA MIGUU YAFANYIKA NCHINI

Image
  Na Mwandishi Maalumu – Dar es Salaam Kwa mara ya kwanza Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) imefanya upasuaji wa kuzibua mishipa ya damu ya miguu iliyoziba kwa wagonjwa 100 wenye matatizo hayo kwa kutumia mtambo wa Cathlab kuzibua mishipa hiyo. Matibabu hayo yamefanyika katika kambi maalumu ya matibabu ya siku tano inafanywa na madaktari bingwa wa moyo wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) kwa kushirikiana na  mwenzao kutoka Hospitali ya BLK iliyopo nchini India. Akizungumzia kuhusu kambi hiyo Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt. Peter Kisenge alisema hadi leo tayari wagonjwa 40 wameshapatiwa matibabu na hali zao kuendelea vizuri ambapo baadhi ya wagonjwa tayari wameruhusiwa. Dkt. Kisenge ambaye pia ni daktari bingwa wa moyo na mishipa ya damu alisema matatizo ya mishipa ya damu ya miguu kuziba yapo kwa wingi katika jamii na mara nyingi huwapata wagonjwa wa kisukari, wagonjwa wa shinikizo la juu la damu pamoja na watu wanaovuta sana sigara na

WAZIRI MKUU AALIKA WAWEKEZAJI VIWANDA VYA MBOLEA

Image
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akisalimiana na Rais wa Shirikisho la Urusi, Vladimir Putin baada ya Ufunguzi wa Jukwaa la Kimataifa la Uchumi na kibinadamu uliofanywa  na Rais Putin kwenye Kituo cha Mikutano na Maonesho  Expo Forum,  St. Petersburg nchini humo Julai 27, 2023. WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewaalika wawekezaji waliobobea kwenye sekta ya mbolea ili waje kufungua viwanda vya mbolea nchini. Ametoa mwaliko huo leo (Alhamisi, Julai 27, 2023) wakati akizungumza kwenye mjadala uliohusu Uimarishaji wa Soko la Mbolea kama njia ya kuondoa njaa barani Afrika uliofanyika kwenye kituo cha mikutano na maonesho cha Expo Forum, jijini St. Petersburg, Urusi. Amesema uamuzi wa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan wa kuongeza bajeti ya kilimo una nia ya kuifanya Tanzania iwe eneo la uzalishaji la kulisha Afrika Mashariki, SADC na bara zima la Afrika. “Bado tuna changamoto ya upatikanaji wa mbolea kwa sababu ikikosekana inaathiri uzalishaji wa chakula.” “Mbolea kwa sasa ndiyo msingi wa uzalishaji cha

KUTOKA MAGAZETINI LEO IJUMAA JULAI 28, 2023

Image