TANAPA YAKUBALI KUANZISHA KITUO KIDOGO CHA ASKARI WA UHIFADHI KATA YA KIHANGA - KARAGWE KUDHIBITI UVAMIZI WA TEMBO.
Karagwe - Kagera. Mbunge wa Jimbo la Karagwe, Innocent Bashungwa amefikia makubaliano na Shirika la Hifadhi ya Taifa Tanzania - TANAPA kuanzisha kituo Kidogo cha askari wa uhifadhi katika kata ya Kihanga wilaya Karagwe ili kudhibiti uharibifu unaofanywa na tembo na wanyama wengine wakali wanaoshambulia Wananchi na mali zao mara kwa mara. Makubaliano hayo yamefikiwa leo tarehe 30, Januari 2023 wakati Bashungwa akisikiliza na kutatua kero za wananchi katika Mkutano wa hadhara uliofanyika Kijiji cha Kibwera kata ya Kihanga wilaya ya Karagwe. Bashungwa ameitaka Halmashauri ya wilaya Karagwe kushirikiana na TANAPA kutoa elimu kwa jamii na kuuunda Vikundi vitakavyokuwa vinashirikana na askari wa Uhifadhi watakaokaa katika kata hiyo kwa ajili ya kulinda usalama wa wananchi na mali zao. Amemtaka Kamishina Msaidizi wa TANAPA Kanda ya ziwa kukamilisha taratibu wa Kulipa fidia kwa wananchi kata Kihanga ambao wameharibiwa mali zao kwa kuvamiwa na tembo ili waweze kupatiwa kifuta machozi kulingana