Posts

RAIS WA ZANZIBAR AMBAE NI MKUU WA CHUO KIKUU CHA TAIFA ZANZIBAR (SUZA) AWATUNUKU WAHITIMU WA MAHAFALI YA 18 SUZA

Image
  RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi ambae pia ni Mkuu wa Chuo Kikuu cha Taifa Zanzibar (SUZA) Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akimtunuku Shahada ya Uzamivu ya Kiswahili  yaani” Doctor of Philosophy in Kiswahili” Nunuu Abdalla Mohammed, wakati wa hafla ya Mahafali ya 18 ya Chuo Kikuu cha Taifa Zanzibar (SUZA) yaliyofanyika katika ukumbi wa Dk.Ali Mohamed Shein Tunguu Wilaya ya Kati Unguja leo 28-12-2022.(Picha na Ikulu)   RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi ambae pia ni Mkuu wa Chuo Kikuu cha Taifa Zanzibar (SUZA) Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akihutubia katika hafla ya Mahafali ya 18 ya Chuo Kikuu cha Taifa Zanzibar (SUZA) mahafali hayo yaliyofanyika katika ukumbi wa Dk.Ali Mohamed Shein Tunguu Wilaya ya Kati Unguja leo 28-12-2022.(Picha na Ikulu) RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi ambae pia ni Mkuu wa Chuo Kikuu cha Taifa Zanzibar (SUZA) Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akiwatunuku wahitimu wa Shahada ya Usimamizi wa Teknolojia ya Habari yaani  

WAZIRI UMMY MWALIMU ATOA WITO KWA WAZAZI NA WALEZI KUSIMAMIA KIKAMILIFU CHANJO KWA WATOTO

Image
  Na Englibert Kayombo, WAF - Dar Es Salaam. Wito umetolewa kwa wazazi na walezi kuhakikisha watoto chini ya miaka mitano (5)wanapata chanjo zote muhimu zinazotolewa ili kuwajengea kinga imara ya kukabiliana na magonjwa yanayozuilika kwa chanjo. Hayo yamesemwa na Waziri wa Afya Mhe. Ummy Mwalimu alipokuwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Temeke Jijini Dar Es Salaam ambapo hivi sasa kuna ongezeko la watoto wanaougua ugonjwa wa Surua. “Nilitoa taarifa kwamba tunaona ongezeko la watoto wenye ugonjwa wa Surua nchini Tanzania na ongezeko hilo tunaliona katika WIlaya ya Temeke, Daktari ametuambia kuwa hapa wanapata watoto wanaougua ugonjwa wa Surua takribani watano kila siku katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Temeke” amesema Waziri Ummy. “Nitoe wito kwa Wazazi na Walezi wenzangu kuhakikisha kwamba watoto wao wanapata chanjo zote muhimu ikiwemo chanjo ya Kifua Kikuu, Polio, na Surua” amesisitiza Waziri Ummy Mwalimu Waziri Ummy amesema kuwa Wizara ya Afya itaweka mpango jumuishi wa kuhak

KATIBU MKUU MPYA WA WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI KASPAR MUYA ARIPOTI OFISINI

Image
  Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Kaspar Kaspar Mmuya akipokea maua kutoka kwa mtumishi wa wizara hiyo,Aisha Juma ikiwa ni ishara ya kumkaribisha Makao Makuu ya wizara hiyo,leo Mtumba jijini Dodoma siku chache baada ya kuapa kuiongoza wizara hiyo.Katikati ni Naibu Katibu Mkuu,Dkt.Maduhu Kazi. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Kaspar Kaspar Mmuya akisalimiana na Mkurugenzi Msaidizi wa Sera na Mipango wa wizara hiyo,Amani Mashaka wakati alipowasili Makao Makuu ya wizara hiyo,leo Mtumba jijini Dodoma siku chache baada ya kuapa kuiongoza wizara hiyo, Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Kaspar Kaspar Mmuya akisalimiana na Mkaguzi Mkuu wa Ndani,Martina Nguluma  wakati alipowasili Makao Makuu ya wizara hiyo,leo Mtumba jijini Dodoma siku chache baada ya kuapa kuiongoza wizara hiyo, Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya N

BARABARA YA MAKETE-MBEYA KUFUNGUKA KWA LAMI

Image
  Barabara ya Makete-Mbeya kufunguka kwa lami Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Prof. Makame Mbarawa amesema Serikali itaendelea na ujenzi wa barabara za lami katika mikoa ya nyanda za juu kusini ili kuunganisha vema ukanda huo na bandari ya Mtwara na hivyo kurahisisha shughuli za usafiri na usafirishaji, kukuza uzalishaji wa mazao ya kilimo, misitu na kukuza utalii. Akizungumza katika hafla ya utiaji saini ujenzi wa barabara ya Isyonje-Kikondo hadi Makete KM 96.2 sehemu ya Kitulo hadi Iniho KM 36.3 inayojengwa kwa kiwango cha lami Waziri Prof. Mbarawa amesema Serikali ya awamu ya sita itahakikisha inaunganisha kwa njia fupi mikoa ya Mtwara, Ruvuma, Njombe hadi Mbeya kupitia Makete ili kukuza fursa za kiuchumi zilizoko katika ushoroba huo. “Serikali inayoongozwa na Rais Dkt. Samia imejikita kwenye kuboreshamiundombinu hususani maeneo yenye uzalishaji mkubwa hivyo niwahakikishie kuwa ongezeni uzalishaji miundombinu bora inakuja,’ amesisitiza Waziri Prof. Mbarawa. Ameitaka Wakala wa Barabara

MAJALIWA AMUWAKILISHA RAIS SAMIA KUMJULIA HALI LOWASSA

Image
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amemwakilisha Dkt. Samia Suluhu Hassan kumjulia hali Waziri Mkuu Mstaafu, Mhe. Edward Ngoyai Lowassa anayeendelea na matibabu Afrika ya  Kusini. Akizungumza na wanafamilia kwa niaba ya Mheshimiwa Rais Samia, Waziri Mkuu amewasilisha salaam za pole kutoka kwa Mheshimiwa Rais na kusema Mheshimiwa Rais anafuatilia hali ya Mheshimiwa Lowassa kwa ukaribu na anamuombea afya njema. Waziri Mkuu ametoa salamu hizo leo (Jumatano, Desemba 28, 2022) jijini Johannesburg, Afrika Kusini ambako alienda kumjulia hali Mheshimiwa Lowassa. Kwa upande wake,  Mke wa Waziri Mkuu Mstaafu, Mama Regina Lowassa amemshukuru Mheshimiwa Rais kwa jinsi ambavyo amekuwa karibu na wanafamilia na namna ambavyo anafuatilia matibabu ya mpendwa wao.   Naye  mtoto mkubwa wa Mheshimiwa Lowassa na Mbunge wa Monduli, Bw. Fredrick Lowassa amewashukuru Watanzania kwa maombi yao ya kumtakia afya njema baba yao. (mwisho) IMETOLEWA NA: OFISI YA WAZIRI MKUU, JUMATANO, DESEMBA 28, 2022. Waziri Mkuu Kassim

SERIKALI KUWAPANGA UPYA WANANCHI WALIOVAMIA ENEO LA HIFADHI NANYUMBU

Image
  Na   Munir Shemweta, WANMM NANYUMBU   Serikali imeamua kuwapanga upya wananchi wa vijiji viwili vya Mbagala Mbuyuni na Marumba wilayani Nanyumbu mkoani Mtwara ili kutatua migogoro ya matumizi ya ardhi na kuleta usalama kwenye maeneo hayo. Akizungumza na wananchi wa kitongoji cha Wanika kata ya Mkonona tarafa ya Nanyumbu wilaya ya Nanyumbu mkoani Mtwara tarehe 28 Desemba 2022 wakati wa ziara ya Mawaziri wa Wizara za Kisekta, Waziri wa Adhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula alisema, kitakachofanyika kila kijiji kitapewa utaratibu utakaosimamiwa na mkuu wa mkoa atakayewapanga wananchi wake na kuyaacha maeneo ambayo si salama kukaliwa na wananchi huku akisisitiza hakuna haki ya mtu itakayopotea. "Mhe Rais anatambua tunayo shule yenye madarasa matatu, na hapa tulipo kuna kaya 94 ambazo ziko hapa na ukienda kitongoji jirani ziko kaya 134 hivyo serikali inajua idadi ya watu kwenye maeneo hayo na mahitaji yao" alisema Dkt Mabula. Aliongeza kuwa, timu ya mawaziri nan

KUTOKA MAGAZETINI LEO ALHAMISI DESEMBA 29, 2022

Image