SERIKALI YAJIPANGA KUIMARISHA USAFIRI MAJINI
WAZIRI wa Ujenzi na Uchukuzi, Prof. Makame Mbarawa amesema Serikali imejipanga kuhakikisha inafanya mapinduzi makubwa katika kuboresha usafiri wa majini kwa kujenga meli na kusomesha wataalam anuai wa fani ya bahari. Akizungumza katika mahafali ya kwanza ya kozi ya ubaharia ambayo yamefadhiliwa na Taasisi ya Ushoroba wa Kati (CCTTFA) jijini Dar es Salaam amewataka wahitimu wa kozi hiyo, kuwa na nidhamu ili ujuzi walioupata uwe na manufaa kwa taifa na nchi za ushoroba wa kati kwa ujumla. “Baharia mzuri ni yule mwenye nidhamu anapokuwa akitekeleza majukumu yake, maono na anayezingatia usalama wake, chombo na mali kwa ujumla,” amesisitiza. Aidha amekitaka Chuo cha Bahari (DMI) kuhakikisha kinakuza mtandao wake na taasisi mbalimbali duniani ili kuwawezesha wanafunzi wa chuo hicho kupata muda wa kutosha wa kufanya mazoezi ya vitendo melini (Sea time). Hata hivyo, Prof. Makame ameupongeza wakala wa ushoroba wa kati kwa kuwafadhili wanafunzi hao na kuahidi kutilia mkazo wa kuwa na mpango