JINSIA, WANAWAKE NA MAKUNDI MAALUM, KWENDA NA VIPAUMBELE NANE, BAJETI YA 2022/23: WAZIRI DKT.GWAJIMA
Na MJJWM, DA ES SALAAM Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Dkt. Dorothy Gwajima, amesema katika Bajeti ya 2022/23, Wizara yake inatazamiwa kwenda na Vipaumbele 8 vitakavyotumia Jumla ya Bil. 43.3 iliyopitishwa na Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Juni. 30. 2022 jijini Dodoma. Dkt. Gwajima ametoa ufafanuzi huo Julai, 30, 2022 wakati akizungumza na Waandishi wa vyombo mbali mbali vya Habari. Waziri Dkt. Gwajima amevitaja vipaumbele hivyo kuwa ni pamoja na kuratibu afua za kukuza usawa wa kijinsia, uwezeshaji wanawake kiuchumi na kiuongozi na kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake, watoto na wazee. Kukuza ari ya jamii kushiriki katika kupanga na kutekeleza miradi ya maendeleo iliyoibuliwa ngazi ya jamii sambamba na kutambua na kuratibu makundi maalum wakiwemo wafanyabiashara ndogondogo (Machinga) ili kuboresha mazingira ya biashara zao. Dkt. Gwajima amesema maeneo mengine ya vipaumbele ni pamoja na kuboresha mazingira ya kufundishia na kujifunzia