Posts

UBALOZI WA MAREKANI WAKUTANA NA WANAFUNZI 70 WALIOKUWA WANASOMA UKRAINE

Image
 Timu ya Ushauri wa Kielimu ya Ubalozi wa Marekani Dar es Salaam (EducationUSA) ilikutana na wanafunzi 70 wa Kitanzania waliorejea kutoka Ukraine baada ya masomo yao kukatishwa na uvamizi wa Urusi. Wanafunzi hao wa shahada ya kwanza wanatafuta fursa ya kuendelea na masomo yao nchini Marekani. Walifahamishwa kuhusu uwezekano wa kusaidiwa na EducationUSA – ambayo ni kitengo ndani ya Ubalozi kinachowasaidia wanafunzi mahiri wa Kitanzania kujiunga na elimu ya juu nchini Marekani. Mkutano huu ulifunguliwa rasmi na Afisa wa Masuala ya Umma wa Ubalozi wa Marekani James Rodriguez ambaye alichangia uzoefu wake wa kuwa mwanafunzi wa shahada ya kwanza nchini Marekani na maisha yake akiwa mfanyakazi wa kujitolewa wa Peace Corps nchini Ukraine miaka michache iliyopita. Katika mkutano huo, Afisa wa Uhamiaji Bi Christa Divis aliwafahamisha wanafunzi hao kuhusu taratibu za uombaji viza za Marekani. Aidha, Mwanafunzi wa Kitanzania anayesoma Chuo Kikuu Connectcut nchini Marekani Bilis Kalolela, kwa njia

KUTOKA MAGAZETINI LEO IJUMAA APRILI 29, 2022

Image
 

NAIBU WAZIRI KUNDO: MSAIDIENI RAIS SAMIA UTEKELEZAJI ANWANI ZA MAKAZI

Image
Immaculate Makilika – MAELEZO, Songwe Naibu Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mheshimiwa Mhandisi, Kundo Mathew amewaomba Wakuu wa Mikoa yote nchini kuendelea kutekeleza zoezi la Anwani za Makazi katika mikoa yao ili kukamilisha zoezi hilo ifikapo Mei 22, 2022. Akizungumza leo mkoani Songwe wakati akiwa katika ziara yake ya kukagua na kuhamasisha utekelezaji wa Operesheni ya Anwani za Makazi, Naibu Waziri huyo alisema kuwa Operesheni Anwani za Makazi inayoendelea kutekelezwa nchini kote ni maelekezo ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan aliyoyatoa Februari 8, 2022, ambapo alielekeza utekelezaji wa Mfumo wa Anwani za Makazi ufanyike kwa Operesheni na ukamilike ifikapo Mei, 2022 chini ya Uratibu wa Wakuu wa Mikoa. “Naomba muendelee kumsaidia Mheshimiwa Rais kwa vile lengo la kukamilisha utekelezaji wa mfumo huu ndani ya muda ulioelekezwa ni kuwezesha Watanzania kupata manufaa yatokanayo na mfumo lakini pia kuwezesha zoezi la

RAIS SAMIA AZINDUA TANZANIA THE ROYAL TOUR JIJINI ARUSHA

Image
Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan akizungumza na Viongozi pamoja na wageni mbalimbali waliohudhuria uzinduzi wa Filamu ya Tanzania The Royal Tour uliofanyika katika ukumbi wa Mikutano wa Arusha International Conference Centre AICC Jijini Arusha tarehe 28, Aprili, 2022.  Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Mwandishi wa Habari Maarufu wa Marekani ambaye ndiye mtayarishaji wa Filamu ya Tanzania The Royal Tour Peter Greenberg mara baada ya kuwasili katika ukumbi wa Mikutano wa Arusha International Conference Centre (AICC). Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan akipokea Tuzo ya Heshima kutoka kwa Rais wa Shirikisho la Filamu Tanzania Eliya Mjatta kuthamini mchango wake katika Tasnia hiyo mara baada ya uzinduzi wa Filamu ya Tanzania The Royal Tour Jijini Arusha 28, Aprili, 2022.   

NSSF YATWAA TUZO YA UTOAJI ELIMU BORA KATIKA KILELE CHA SIKU YA USALAMA NA AFYA MAHALA PA KAZI

Image
  Tuzo hiyo ni kielelezo tosha kuwa NSSF ilifanikiwa kuwafikia baadhi ya wananchi wa Mkoa wa Dodoma na Mikoa ya jirani kwa ufanisi mkubwa. Ahadi ya NSSF ni kuendelea kutumia mikakati mbalimbali kutoa elimu kwa faida ya wanachama kutoka Sekta Binafsi na Sekta Isiyo Rasmi Nchi mzima, ambapo katika Maonesho ya OSHA NSSF inatoa elimu ya hifadhi ya jamii, uelewa kuhusu mifumo na kupokea kero mbalimbali na kuzipatia ufumbuzi. Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF), Masha Mshomba akipokea Tuzo ya kundi la watoa Elimu bora kutoka kwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Dkt. Profesa Joyce Ndalichako katika maonesho ya OSHA yanayoendelea jijini Dodoma Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Taifa  wa Hifadhi ya Jamii (NSSF), Masha Mshomba akitoa maelezo kwa Waziri Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe.Profesa Joyce Ndalichako, kuhusu kazi zinazofanywa na NSSF katika Maonesho ya OSHA yanayoendelea Mkoani Dodoma

SEKTA BINAFSI KUNUFAIKA NA MIKOPO BENKI YA DUNIA

Image
Na Benny Mwaipaja, Washington DC TANZANIA inatarajia kupata dola za Marekani milioni 200 sawa na shilingi za Tanzania, bilioni 460 kutoka Benki ya Dunia kupitia Taasisi yake inayoshughulika na utoaji wa mikopo na misaada kwenye Sekta Binafsi – International Finance Corporation (IFC), kwa ajili ya kusaidia utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo kupitia sekta binafsi. Hayo yamesemwa na Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Emmanuel Tutuba baada ya kukutana na kufanya mazungumzo na Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia wa Taasisi inayoshughulika na utoaji mikopo na misaada kwenye Sekta Binafsi (International Finance Corporation-IFC), Kanda ya Afrika, Bw. Sergio Pimenta, Jijini Washington DC, Marekani. Bw. Tutuba alisema kuwa fedha hizo zittumika kuendeleza shughuli za uzalishaji kwenye viwanda, maendeleo ya tehama na kusaidia miradi ya wanawake, wenye ulemavu na vijana kupitia taasisi mbalimbali za fedha. Alisema kuwa uwekezaji wa Benki ya Dunia kwenye Sekta binafsi kupiti

PSSSF YATWAA TUZO KILELE CHA SIKU YA AFYA NA USALAMA MAHALI PA KAZI

Image
NA MWANDISHI WETU, DODOMA MFUKO wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF) umepewa tuzo ya kutoa huduma rafiki kwa wazee na wagonjwa wakati wa Maonesho ya Siku ya Usalama na Afya Mahali pa Kazi Duniani iliyofanyika kwenye viwanja vya Kituo cha Mikutano Jakaya Kikwete jijini Dodoma. Aliyekabidhi tuzo hiyo ni mgeni rasmi katika sherehe hizo Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe. Prof. Joyce Lazaro Ndalichako na ilipokelewa na Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu, PSSSF, Paul Kijazi. Siku ya usalama na afya mahali pa kazi Duniani ni siku ya Kimataifa ya kufanya kampeni ya kuboresha usalama na afya ya wafanyakazi,  lengo ni kuondoa hali zote hatarishi mahali pa kazi na hivyo kuifanya kazi iwe ya hadhi na heshima na hufanyika kila mwaka kuelekea Siku ya Wafanyakazi Duniani yaani Mei Mosi. Kwa mujibu wa Afisa Uhusiano Mkuu wa PSSSF, Abdul Njaidi alisema ushiriki wa Mfuko kwenye maonesho hayo  ilikuwa ni fursa nzuri ya kukutana na wanachama

MHE. JENISTA AFUTURISHA WAKE WA VIONGOZI WAKUU KITAIFA WASTAAFU

Image
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Jenista Mhagama  akiwakaribisha wake wa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mstaafu, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, Zakia na Asha kushiriki nao kwenye futari aliyoiandaa kwa wake wa Viongozi Wakuu wa Kitaifa wastaafu jijini Dar es salaam. Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Jenista Mhagama akifafanua jambo kwa wake wa Viongozi Wakuu wa Kitaifa wastaafu alipojumuika nao kwenye futari aliyoiandaa jijini Dar es salaam. Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Jenista Mhagama  akiwakaribisha wajane wa aliyekuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Hayati Edward Moringe Sokoine, Mama Napono na Nakiteto kushiriki nae kwenye futari aliyoiandaa. Nyuma yake ni Naibu Waziri wa Ofisi yake Mhe. Deogratius Ndejembi na Naibu Katibu Mkuu, Bw. Xavier Daudi. Wake wa Viongozi Wakuu wa Kitaifa wastaafu wakiw