Posts

SPIKA WA BUNGE AKUTANA NA BALOZI WA UGANDA NCHINI

Image
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Tulia Ackson akizungumza na Balozi wa Uganda nchini Tanzania, Mhe. Richard Mabonero leo Machi 30, 2022 ofisini kwake Bungeni Jijini Dodoma. Balozi huyo amemtembela Mhe. Spika kwa lengo la kumuaga baada ya kumaliza muda wake wa kufanya kazi hapa nchini.  Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Tulia Ackson katika picha ya pamoja na Balozi wa Uganda nchini Tanzania, Mhe. Richard Mabonero leo Machi 30, 2022 ofisini kwake Bungeni Jijini Dodoma. Balozi huyo amemtembela Mhe. Spika kwa lengo la kumuaga baada ya kumaliza muda wake wa kufanya kazi hapa nchini.(PICHA NA OFISI YA BUNGE)

RAIS SAMIA APOKEA RIPOTI ZA TAKUKURU NA CAG ZA MWAKA 2020/2021

Image
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akipokea Taarifa ya Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU). kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi hiyo Kamishna wa Polisi (CP) Salum Hamduni katika hafla iliyofanyika Ikulu Chamwino Jijini Dodoma leo tarehe 30 Machi, 2022. RAIS pia akipokea ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Serikali (CAG). Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan akizungumza na viongozi mbalimbali mara baada ya kupokea Taarifa ya Ukaguzi wa Hesabu za Serikali kwa mwaka 2020/2021 pamoja na Taarifa ya Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), katika hafla iliyofanyika Ikulu Chamwino. Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan akizungumza na viongozi mbalimbali mara baada ya kupokea Taarifa ya Ukaguzi wa Hesabu za Serikali kwa mwaka 2020/2021 pamoja na Taarifa ya Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), katika hafla iliyofanyika Ikulu Chamwino. Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan akizungumza na viongozi mbalimbali mara baada ya kupokea Taarifa ya U

WIZARA YA ARDHI YASHIRIKIANA NA KOREA KUBADILISHA MIFUMO YAKE KUWA YA KIDIGITALI

Image
 Na  Munir Shemweta, WANMM DODOMA Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa ushirikiano wake na Korea Kusini imeanzisha mkakati wa kuhakikisha inabadilisha mifumo yake upangaji, utumiaji, upimaji na uwekaji kumbukumbu za sekta ya ardhi kutoka analogia kwenda digitali ili kuboresha sekta ya ardhi. Hatua hiyo inafuatia mifumo mingi ya upangaji, utumiaji upimaji na uwekaji kumbukumbu za ardhi katika Wizara ya Ardhi kuendelea kutumia mifumo ya analogia katika upangaji, utumiaji, upimaji na uwekaji kumbukumbu za sekta ya ardhi. Katika kufanikisha azma hiyo Serikali ya Tanzania kupitia Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi pamoja na Serikali ya Korea Kusini zimeingia makubaliano ya ushirikiano wa utekelezaji mradi wa ujenzi wa kituo cha Kisasa cha Mafunzo pamoja na uboreshaji miundombinu ya sekta ya ardhi. Hayo yamebainishwa tarehe 30 Machi 2022 jijini Dodoma na Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Allan Kijazi wakati akielezea ushirikiano baina ya se

SERIKALI YAFUTA TOZO 42 ZAO LA KAHAWA-MAJALIWA

Image
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ametangaza uamuzi wa Serikali wa kuondoa tozo 42 kati ya 47 ambazo walikuwa wanatozwa wakulima wa kahawa wa Mkoa wa Kagera hadi kufikia tozo 5 tu ambazo itakuwa ni jumla ya Shilingi 267 kwa kila kilo ya kahawa, kutoka Shilingi 830 za awali. Waziri Mkuu ametoa maamuzi hayo kufuatia tume maalum aliyoiunda ili kupitia utaratibu na mfumo wa uendeshaji wa vyama vya Ushirika wa zao la kahawa Mkoani Kagera. Mheshimiwa Majaliwa amewaagiza viongozi wa vyama vya Ushirika, wasimamie vyama vyao kwa uaminifu na weledi ili vilete tija kwa wakulima. Pia, Mheshimiwa Majaliwa amewata viongozi wa vyama vikuu vya ushirika kuacha tabia ya kukopa pesa benki kwa ajili ya kununua kahawa kwa wakulima. Waziri Mkuu ameyatoa maagizo hayo leo (Jumanne, Machi 29, 2022) Wakati alipoendesha Mkutano Maalum wa Wadau wa zao la kahawa mkoani Kagera uliofanyika wilayani Karagwe Mkoa wa Kagera. Amesema kuanzia sasa mauzo ya kahawa katika Mkoa wa Kagera yatafanyika kwa njia ya mnada. “Mnada huo

TANZANIA YAJIPANGA KUTUMIA WANAHABARI KUFIKIA MAAZIMIO YA MALABO

Image
  Meneja wa Kituo cha Utafiti cha TARI Mikocheni Dkt.Joseph Ndunguru akifungua mafunzo hayo ya kitaifa ya siku nne kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa TARI. Afisa Programu ya CAADP -XP4, Bi. Futh Magagula akitoa salamu za Taasisi ya Uratibu wa Tafiti za Kilimo Afrika (CCARDESA) wakati wa ufunguzi wa mafunzo hayo jijini Dar es salaam. Meneja wa Mawasiliano na menejimenti ya Maarifa kutoka Taasisi ya Utafiti Tanzania (TARI) Dkt. Richard Kasuga akieleza malengo ya Mafunzo hayo ya Kiataifa ya siku nne kwa Maafisa mawasiliano, Wanahabari na wadau wengine. Afisa Habari na Menejiment ya Maarifa kutoka kutoka Taasisi ya Uratibu wa Tafiti za Kilimo Afrika (CCARDESA) Bi. Bridget Kakulwa akieleza akieleza matarajio ya Mafunzo hayo. Bwana Shadrack Ndalawa msimamizi wa dawati la CAADP Wizara ya Kilimo akieleza utekeeleaji wa maazimio Malabo upande wa Tanzania Washiriki wa Mafunzo hayo wakifuatilia Hotuba za ufunguzi.   Washiriki wa Mafunzo hayo wakifuatilia Hotuba za ufunguzi.   Washiriki wa Mafunzo ha

WAZIRI DKT. NDUMBARO AKUTANA NA BALOZI WA MAREKANI NCHINI

Image
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Damas Ndumbaro (kulia), akizungumza na Balozi wa Marekani Nchini, Dkt. Donald Wright kuhusu masuala mbalimbali ya Uwekezaji Mahiri katika Vitalu vya Uwindaji wa Wanyamapori . Kikao hicho kimefanyika leo Jijini Dar es Salaam Picha na WMU. Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Damas Ndumbaro (kulia), akiagana na Balozi wa Marekani Nchini, Dkt. Donald Wright mara baada ya kufanya mazungumzo kuhusu masuala mbalimbali ya Uwekezaji Mahiri katika Vitalu vya Uwindaji wa Wanyamapori . Kikao hicho kimefanyika leo Jijini Dar es Salaam  Picha na WMU. Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Damas Ndumbaro (kulia), akiwa kwenye picha ya pamoja mara baada ya kufanya mazungumzo na Balozi wa Marekani Nchini, Dkt. Donald Wright kuhusu masuala mbalimbali ya Uwekezaji Mahiri katika Vitalu vya Uwindaji wa Wanyamapori . Kikao hicho kimefanyika leo Jijini Dar es Salaam

KUTOKA MAGAZETINI LEO JUMATANO MACHI 30, 2022

Image