Posts

KUTOKA MAGAZETINI LEO IJUMAA JANUARI 28, 2022

Image
 

RAIS SAMIA ASHEREHEKEA SIKU YAKE YA KUZAALIWA

Image
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akikata keki kama ishara ya kusherehekea kumbukumbu ya siku yake ya kuzaliwa leo tarehe 27 Januari, 2022 Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma.  

WAZIRI BASHUNGWA AMPONGEZA MKURUGENZI WA DART DK.EDWIN MHEDE KWA KUONGEZA MAPATO

Image
  WAZIRI wa Nchi Ofisi Rais Tawala za Mikoa (TAMISEMI) Innocent Bashungwa akizungumza na na  Menejimenti ya taasisi  ya Wakala wa Mabasi yaendayo Haraka(DART)  alipofanya ziara katika Ofisi za Wakala hiyo pamoja na kutembelea miundombinu inayotoa huduma na ile inayoendelea kujengwa, ili kuona mapato na maendeleo ya mradi kushoto anayemsikiliza ni Mkurugenzi wa Wakala wa Mabasi yaendayo Haraka(DART) Dk. Edwin Mhede. Picha mbalimbali zikionesha Wazriri  wa Nchi Ofisi Rais Tawala za Mikoa (TAMISEMI) Innocent Bashungwa, Mkurugenzi wa Wakala wa Mabasi yaendayo Haraka(DART) Dk. Edwin Mhede na Naibu Katibu Mkuu anayeshughulikia Afya Ofisi ya Rais TAMISEMI Dkt. Grace Magembe wakipata maelezo kutoka kwa Mohamed Kuganda Kaimu Mkurugenzi wa Maendeleo ya Usafirishaji DART wakati alipokagua miundombinu ya shirika hilo. Wazriri  wa Nchi Ofisi Rais Tawala za Mikoa (TAMISEMI) Innocent Bashungwa kulia na Mkurugenzi wa Wakala wa Mabasi yaendayo Haraka(DART) Dk. Edwin Mhede kwa pamoja wakati w

MAJALIWA: WATANZANIA TUSHIKAMANE KUIPA THAMANI TANZANITE

Image
 WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewataka watanzania kushirikiana na kushikamana ili kuyapa thamani madini ya Tanzanite na kuifanya dunia nzima itambue kuwa madini ya Tanzanite yanapatikana Tanzania tu na tayari imeweka mazingira ya kuyaongezea thamani. Mheshimiwa Majaliwa ameyasema hayo leo (Jumatano, Januari 26, 2022) alipozungumza na wananchi katika eneo la EPZA unapojengwa Mji wa Tanzanie katika Mji Mdogo wa Mirerani wilayani Simanjiro akiwa katika ziara ya kukagua miradi ya maendeleo mkoani Manyara. Waziri Mkuu amesema Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan itahakikisha rasilimali zote zilizoko nchini yakiwemo madini ya Tanzanite zinawanufaisha wananchi wote hususani wanaoishi katika maeneo zinapopatikana. “Watanzania lazima tushirikiane na tushikamane kuyapa thamani madini hayo.” Amesema kuwa Serikali itaendelea kukutana na wafanyabiashara wa sekta madini kwa lengo la kuhakikisha kwa pamoja wanaweka mikakati ya kusaidia kuikuza sekta hiyo ili i

RAIS SAMIA AKUTANA NA MAKAMU WA KWANZA WA RAIS WA ZANZIBAR IKULU JIJINI DAR ES SALAAM

Image
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Othman Masoud Othman mara baada ya kuwasili Ikulu Jijini Dar es Salaam leo tarehe 26 Januari, 2022.

KUTOKA MAGAZETINI LEO JUMATANO TAREHE 26/1/2022

Image