BASHUNGWA ATAKA MICHEZO YA WENYE ULEMAVU KUWA MICHEZO YA KIPAUMBELE
Na. John Mapepele, WUSM Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo. Mhe, Innocent Bashungwa amewaagiza Watendaji Wote, wa Sekta ya michezo kuhakikisha michezo ya wenye ulemavu, hususan soka kuwa miongoni mwa michezo ya kipaumbele na kuitaka kuingizwa kwenye mifumo rasmi, ya kukuza vipaji, kama UMITASHUMTA na UMISSETA. Mhe. Bashungwa ameyasema hayo leo Novemba 27, 2021 wakati alipokuwa akifungua mashindano ya Afrika ya Mpira wa Miguu kwa watu Wenye ulemavu kwa wanaume (CANAF 2021) katika Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam. “Serikali ya Awamu ya Sita, chini ya Mhe. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, inatambua thamani na fursa zilizopo katika michezo yote, ikiwemo kundi la watu wenye ulemavu. Kwa msingi huo tumechukua jukumu hili, ili kuhakikisha fursa hii inatumika vema kuiweka timu yetu ya soka ya Taifa kwa walemavu, ya Tembo katika ramani ya mchezo huu kimataifa”. Amefafanua Mhe Bashunga Akimkaribisha kufungua mashindano hayo, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya U