Benki Kuu ya Tanzania imelipongeza Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) kwa hatua iliyofikia ya kuanza usafishaji wa dhahabu hapa nchini kwa ubora wa kimataifa. Pongezi hizo zimetolewa na Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania, Prof. Florens Luoga, (pichani juu)wakati alipotembelea kiwanda cha kusafisha dhahabu cha Mwanza Precious Minerals Limited, kilichopo jijini Mwanza Ijumaa na kujionea maendeleo yaliyofikiwa hadi sasa, ikiwemo kuanza uzalishaji. “Haya ni mapinduzi makubwa katika sekta ya madini na ukombozi kwa wachimbaji, wafanyabiashara na wadau wengine wa sekta hii. Ndoto ya Tanzania kuacha kusafirisha dhahabu ghafi naona inaelekea kutimia”, alisema Gavana Luoga. Aidha, Prof. Luoga alivutiwa na taarifa kwamba kiwanda hicho ambacho kinamilikiwa kwa ubia kati ya serikali kupitia STAMICO na wawekezaji wa nje, pia kina uwezo wa kutenganisha dhahabu na madini mengine ambayo yana thamani katika masoko ya madini duniani. “Kwa uwezo wa kiwanda hiki, nina imani mtaweza kununua dhahabu