Posts

IGP SIRRO AZINDUA KITABU CHA MUONGOZO WA KUZUIA NA KUFICHUA UHALIFU,

Image
  MKUU wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro amewataka watu wanaopata msamaha wa vifungo kutoka gerezani kuacha kujihusisha na uvunjifu wa amani ikiwa pamoja na kuacha kujiingiza tena kwenye matukio ya uhalifu na badala yake wajikite katika kuleta maendeleo kwenye jamii. IGP Sirro amesema hayo leo wakati akizindua kitabu cha muongozo wa kufichua na kuzuia uhalifu kitabu ambacho kinalenga kutoa dira hasa katika utekelezaji wa mpango wa Polisi kata kupitia mpango mkakati wa ushirikishwaji wa jamii

PICHA: NAIBU SPIKA DKT. TULIA AKUTANA NA KUFANYA MAZUNGUMZO NA WATENDAJI KUTOKA NMB BENKI JIJINI DODOMA

Image
Naibu Spika wa Bunge, Mhe. Dkt. Tulia Ackson (watatu kushoto) katika picha ya pamoja na Watendaji wa Benki ya  NMB wakiongozwa na  Mkurugenzi  Mkuu  wa Benki hiyo, Ndg. Ruth Zaipuna (watatu kulia) walipomtembelea leo katika ofisi za Bunge Jijini Dodoma. Naibu Spika wa Bunge, Mhe. Dkt. Tulia Ackson (kulia) akizungumza na Mkurugenzi  Mkuu  wa Benki ya  NMB , Ndg. Ruth Zaipuna alipomtembelea leo katika ofisi za Bunge Jijini Dodoma. Naibu Spika wa Bunge, Mhe. Dkt. Tulia Ackson (kushoto) akifurahi jambo na Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya NMB, Ndg. Ruth Zaipuna alipomtembelea leo katika ofisi za Bunge Jijini Dodoma. Wageni wengine ni watendaji kutoka Benki hiyo  

HALMASHAURI KUU YA TAIFA YA CCM YAKETI JIJINI DODOMA

Image
  Wajumbe mbalimbali wa NEC wakiwa katika Kikao hicho cha NEC kilichofanyika leo tarehe 29 Aprili, 2021 katika Makao Makuu cha Chama White House Jijini Dodoma. PICHA NA IKULU. Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi CCM (Bara) Rodrick Mpogolo akizungumza katika Kikao cha Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama cha Mapinduzi CCM (NEC) kilichofanyika leo tarehe 29 Aprili, 2021 katika Makao Makuu cha Chama, White House Jijini Dodoma. Kikao hicho kimehudhuriwa na Mjumbe wa NEC Taifa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan, Makamu Mwenyekiti wa CCM (Zanzibar) Dkt. Ali Mohamed Shein pamoja na Makamu Mwenyekiti CCM Tanzania Bara Philip Mangula  Mjumbe wa NEC Taifa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akiwa katika kikao hicho cha Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama cha Mapinduzi CCM (NEC) kilichofanyika leo tarehe 29 Aprili, 2021 katika Makao Makuu cha Chama White House Jijini Dodoma. Makamu Mwenyekiti wa CCM (Zanzibar) Dkt. Ali M

WAZIRI PROF MKENDA APIGA MARUFUKU POLISI KUKAMATA WAFANYABIASHARA WA MAHINDI

Image
  WAZIRI wa Kilimo Prof. Aldof Mkenda amepiga marufuku kwa jeshi la polisi kukamata wafanyabiashara ya mahindi wakati wanapeleka bidhaa yao sokoni kwani hali hiyo inakatisha tamaa wakulima. Prof.Mkenda ametoa Kauli  wakati wa ziara yake ya kikazi ya kukagua na kujionea  Mashamba ya Kilimo cha mkataba wa zao la mtama wilayani Kongwa. Waziri Mkenda amesema kuwa anatarajia kuzungumza na Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP) kuhakikisha Jeshi hilo linaachana na tabia ya kukimbizana na wafanyabiashara hao wakati wakipeleka biashara zao sokoni. "Kuna changamoto kubwa ya masoko inayowakabili wafanyabiashara wa mahindi nchini, wafanya biashara hao wanauhuru wa kufanya biashara eneo lolote nchini kwa kuwa wanakuwa wakitafuta masoko, hivyo kuwazuia na kuwanyang’anya mazao yao wakati wakipeleka sokoni ni kuwavunja moyo na kuwakatisha tamaa,”amesema Prof.Mkenda. Hata hivyo Prof. Mkenda amewataka askari wa Jeshi la Polisi nchini kuacha tabia hiyo ya kuwanyanyasa na kuwasumbua wakulima na wafany

WCF YAZOA TUZO KATIKA MAONESHO YA USALAMA NA AFYA MAHALI PA KAZI (OSH 2021)

Image
 WCF YAZOA TUZO KATIKA MAONESHO YA USALAMA NA AFYA MAHALI PA KAZI (OSH 2021)  Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF) umezoa tuzo katika kilele cha maadhimisho ya Wiki ya Usalama na Afya mahali pa kazi duniani baada ya kuibuka kinara wa kundi la Taasisi za bima na Taasisi bora ya Umma inayosimamia vizuri masuala ya usalama na afya mahali pa kazi.  Akikabidhi tuzo hizo wakati wa kilele cha Maadhimisho ya Wiki ya Usalama na Afya mahali pa kazi duniani yanayofanyika jijini Mwanza kitaifa, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Kazi, Vijana, Ajira na wenye Ulemavu, Mhe. Jenista Mhagama (MB) alitoa rai kwa Mfuko kuendelea kushirikiana na Wakala wa salama na Afya mahali pa kazi (OSHA) ili kuboresha ufanisi katika utendaji kazi. “WCF endeleeni kushirikiana na OSHA katika programu mbalimbali ili kupunguza ajali, magonjwa na vifo vinavyotokana na kazi. Badilishaneni taarifa za muhimu ambazo zitasaidia kuboresha utendaji wenu kwa sababu mmoja anasimamia mazingira salama ya kufanyia k

MCHUNGAJI WA KANISA LA BAPTIST NYANHENDE AMWAGA MSAADA KWA WATOTO WENYE UALBINO BUHANGIJA

Image
    Mchungaji wa Kanisa la Baptist Nyanhende Manispaa ya Shinyanga Renatus Kanunu, akikabidhi msaada wa vitu mbalimbali kwa watoto wenye mahitaji maalumu wanaolelewa kituo cha Buhangija , kikiwemo chakula.

DARAJA LA KIYEGEYA MBIONI KUKAMILIKA

Image
Meneja wa TANROADS, mkoa wa Morogoro, Mhandisi, Kolante Ntije, akimuonesha Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Mhandisi, Dkt. Leonard Chamuriho (mwenye tai), mihimili mikuu itakayowekwa kwenye daraja la Kiyegeya, mkoani Morogoro, wakati Waziri huyo alipofika darajani hapo kujionea maendeleo yake. Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Mhandisi, Dkt. Leonard Chamuriho (mwenye tai), akiangalia mihimili mikuu itakayowekwa kwenye daraja la Kiyegeya, mkoani Morogoro, wakati Waziri huyo alipofika darajani hapo kujionea maendeleo yake. Muonekano wa mihimili mikuu itayowekwa katika daraja la Kiyegeya ikiwa imekamilika.  Muonekano wa moja ya nguzo zitakazoshikilia daraja la Kiyegeya ikiwa katika hatua za mwisho kukamilika.PICHA NA WUU Serikali imesema inatarajia kukamilisha ujenzi wa daraja la Kiyegeya, mkoani Morogoro, hivi karibuni, ambalo lilibomoka mwezi Machi, mwaka jana kutokana na mvua kubwa zilizokuwa zikinyesha. Akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa daraja hi

BARAZA LA MADIWANI MANISPAA YA IRINGA LIMEPITISHA UTARATIBU MPYA WA WA VITUO VYA KUPAKIA ABILIA NA NJIA ZA BAJAJI NA DALADALA

Image
  Mstahiki Meya wa manispaa ya Iringa Ibrahim Ngwada akisoma maazimio yaliyotewa na madiwani wa manispaa ya Iringa wakati wakijadili namna ya kutatua mgomo wa daladala na bajaji  Baadhi ya madiwani wakiwa kwenye baraza maalumu kwa ajili ya kutafuta njia ya kutatua mgomo wa daladala na bajaji Baadhi ya madiwani wakiwa kwenye baraza maalumu kwa ajili ya kutafuta njia ya kutatua mgomo wa daladala na bajaji Na Fredy Mgunda Iringa. Baraza la madiwani manispaa ya Iringa limepitisha utaratibu mpya wa wa vituo vya kupakia abilia na barabara zitakazo kuwa zinatumiwa na bajaji na daladala zote za manispaa ya Iringa kwa lengo la kutatua mgogoro uliokuwepo baina ya daladala na bajaji. Akitoa maazimio hayo mbele ya baraza maalum la madiwa lililofanyika tarehe 28 mwezi wa nne mstahiki meya wa manispaa ya Iringa Ibrahim Ngwada alisema   kuwa baraza limetafuta njia ya kutatua mgogoro huo kwa kuangalia namna bora ya njia na vituo ambavyo vitatumika. Alisema kuwa bajaji zote za zamani zinazotoka

KUTOKA MAGAZETINI LEO ALHAMISI APRILI 29, 2021

Image