Posts

KANISA HALISI LAMUOMBEA MAKUBWA RAIS SAMIA, LAMKABIDHI MUNGU BABA KAZI ALIZOFANYA HAYATI DK. MAGUFULI AMKABIDHI RAIS HUYO KUZIENDELEZA

Image
  Baba Halisi wa Uzao akiendesha Sala Maalum ya Kulivusha Taifa la Tanzania, iliyofanyika jana kwenye Viwanja vya Mwanga Community Centre, Mwanga mkoani Kigoma . Na Bashir Nkoromo, CCM Blog Kanisa Halisi la Mungu Baba la Tegeta jijini Dar es Salaam, limefanya Ibada ya 'Kulivusha Taifa', ambapo  limemuomba Mungu Baba kumuinua Rais Samia Suluhu Hassan na kumpa ulinzi wake dhidi ya wabaya, afya njema na hekima ya ajabu ili aweze kutenda vema kazi yake ya kuliongoza Taifa la Tanzania. Pia katika ibada hiyo, Kanisa Halisi la Mungu Baba limemkabidhi Mungu Baba kazi zote alizofanya aliyekuwa Rais wa Tanzania Hayati Dk. John Magufuli, azichukue na kuzikabidhi yeye mwenyewe Mungu kwa baraka zote kwa Rais Samia Suluhu Hassan ili kuziendeleza. Hayo yamejiri katika Ibada hiyo Maalum ya 'Kulivusha Taifa'  iliyofanyika kuanzia saa nane mchana hadi saa kumi jioni ikiongozwa na Kiongozi wa Kanisa hilo Baba Halisi wa Uzao, kwenye Viwanja vya Mwanga Community Centre, Mwanga mkoani Kigoma

KUTOKA MAGAZETINI LEO JUMATATU MACHI 29, 2021

Image
 

RAIS SAMIA APOKEA RIPOTI ZA MWAKA 2019/2020 ZA CAG NA TAKUKURU

Image
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akimsikiliza Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) Charles Kichere wakati akitolea maelezo moja ya Taarifa zake za ukaguzi leo tarehe 28 Machi 2021 katika Ikulu ya Chamwino mkoani Dodoma. Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) Charles Kichere akionesha moja ya Taarifa zake za ukaguzi wa Hesabu za Serikali kwa mwaka wa fedha 2019/20 kabla ya kuziwasilisha kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan leo tarehe 28 Machi 2021 katika Ikulu ya Chamwino mkoani Dodoma. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akimsikiliza Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU Brigedia Jenerali John Mbungo wakati akitolea Maelezo moja ya Taarifa yake ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa kwa mwaka 2019/20 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akielekea katika ukumbi wa Mikutano wa Ikulu ya Chamwino mkoani Dodoma kwa ajili ya kupokea Ta

RAIS SAMIA "AMTUMBUA" MKURUGENZI MKUU TPA DEUSDEDIT KAKOKO

Image
 RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, amemsimamisha kazi MKURUGENZI MKUU wa Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) Bw. Deusdedit Kakoko ili kupisha uchunguzi. Rais Samia ametangaza uamuzi huo leo Machi 28, 2021 wakati akipokea ripoti ya mdhibiti na mkaguzi MKUU wa hesabu za serikali (CAG) ya mwaka 2019/2020 na ile ya Taasisi ya Kuzuia na kudhibiti Rushwa (TAKUKURU) Ikulu ya Chamwino jijini Dodoma leo Machi 28, 2021.

KUTOKA MAGAZETINI LEO JUMAPILI MACHI 28, 2021

Image
 

NEC YATANGAZA UCHAGUZI MDOGO WA UBUNGE JIMBO LA MUHAMBWE, KIGOMA

Image
  Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Dkt. Willson Mahera   Na Mwandishi Maalum, Dodoma TUME ya Taifa ya Uchaguzi imetangaza Ratiba ya uchaguzi mdogo wa Ubunge wa Jimbo la Muhambwe, mkoani Kigoma baada ya kupokea Barua kutoka kwa Spika wa Bunge kuwa kiti hicho kiko wazi. Taarifa iliyotolewa kwa Vyombo vya habari Jijini Dodoma leo, 27 Machi, 2021, na kusainiwa na Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Dkt. Willson Mahera amesema uchaguzi huo umeapangwa kufanyika tarehe 2 Mei,2021. “Tume ilipokea barua kutoka kwa Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ambaye kwa kuzingatia kifungu cha 37 (3) cha Sheria ya Taifa ya Uchaguzi, Sura ya 343, ameitaarifu Tume uwepo wa nafasi wazi ya kiti cha Ubunge katika Jimbo la Muhambwe, Halmashauri ya Wilaya ya Kibondo, Mkoani Kigoma,” alisema Dkt Mahera.   Aidha, kwa kuzingatia kifungu cha 37 (1) (b), cha Sheria ya Taifa ya Uchaguzi, sura ya 343 ambacho kinaitaka Tume kujaza nafasi ya kiti cha Ubunge ka

MATUKIO YA PICHA MAZISHI YA JPM HUKO CHATO MACHI 26, 2021

Image