WAZIRI AWESO AAGIZA MKANDARASI KULIPWA FEDHA
Mh.Waziri akimtwisha ndoo mmoja wa wananchi wa kijiji cha kashangu Halmashauri ya Itigi mara baada ya kuzindua mradi huo. Waziri na watendaji wa RUWASA pamoja na Viongozi wengine wa Wilaya ya Manyoni wakipanda juu ya Tanki la maji linalohudumiwa na mradi wa kintinku. iongozi akiwemo Pius Chaya katikati wakiongozana na Mh.Waziri kutoka kwenye chanzo cha maji katika mradi wa kintinku Wilayani Manyoni.. Waziri akiteta jambo na Meneja wa RUWASA Mhandisi Lucas Said. Mh.Waziri akizungumza mara baada ya kukagua chanzo cha mradi wa kintinku Wilayani Manyoni. Na Mwandishi wetu,Singida. WAZIRI wa Maji, Jumaa Aweso ametoa siku saba kwa Meneja wa wakala wa maji na usafi wa Mazingira Vijijini na mijini (RUWASA) Mkoa wa Singida kumlipa Mkandarasi anayejenga mradi wa maji uliopo katika Kijiji cha Kintinku Wilayani Manyoni. Aweso alitoa kauli hiyo juzi wakati wa ziara yake ya kikazi ya siku moja mkoani hapa ya kutembelea miradi pamoja na kuzungumza na wafanyakazi wa idara hiyo ya maji. Baada ya W