Posts

JPM AZINDUA MIRADI YA KIHISTORIA TABORA, NI WA MAJI NA UJENZI WA JENGO LA IMEJENSI HOSPITALI YA RUFAA YA MKOA

Image
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Waziri wa Afya Dkt. Dorothy Gwajima, Mawaziri pamoja na viongozi wengine wakati akiweka jiwe la msingi ujenzi wa jengo la Idara ya Wagonjwa wa Huduma ya Dharura katika Hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Tabora leo tarehe 30 Januari 2021.  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akimsikiliza Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji Mhandisi Anthony Sanga wakati akikagua ujenzi wa Matanki makubwa ya kuhifadhia maji katika mradi mkubwa wa maji ya Ziwa Victoria katika miji ya Tabora, Igunga na Nzega Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Wananchi wa mkoa wa Tabora katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika uwanja wa Ali Hassan Mwinyi mkoani Tabora leo tarehe 30 Januari 2021 mara baada ya kuzindua mradi wa maji ya kutoka ziwa Victoria pamoja na jengo la huduma kwa wagonjwa wa dharura.  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiw

NAIBU WAZIRI MARY FRANCIS AONGOZA MAZOEZI WILAYANI MAGU

Image
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Mary Francis Masanja ( wa pili kutoka kushoto mbele) akiongoza mazoezi ya kutembea na kukimbia yaliyowahusisha wananchi na viongozi mbalimbali wa Halmashauri ya Wilaya ya Magu akiwemo Mkuu wa Wilaya hiyo Mhe. Salum Kalli (,) leo tarehe 30/1/2021. Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Mary Francis Masanja akizungumza na wananchi wa Wilaya ya Magu mara baada ya  kuongoza mazoezi ya kutembea na kukimbia yaliyowahusisha pia viongozi wa Halmashauri hiyo. Mkuu wa Wilaya ya Magu, Mhe. Salum Kalli akiongea na Wananchi mara baada ya kuhitimisha  mazoezi ya kutembea na kukimbia yaliyowahusisha wananchi na viongozi na Watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Magu leo Januari 30, 2021.  

NAIBU WAZIRI KUNDO ATOA WITO KWA BARAZA LA WAFANYAKAZI

Image
Na Faraja Mpina - WMTH Wito umetolewa kwa wajumbe wa Baraza la wafanyakazi wa Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi na kutoa huduma bora kwa kuzingatia vigezo walivyojiwekea. Wito huo umetolewa na Naibu Waziri wa Wizara hiyo  Mhandisi Andrea Kundo wakati akifungua Mkutano wa Baraza la wafanyakazi wa wizara hiyo jijini Dodoma,ambapo amesema ili kutekeleza malengo ya wizara hiyo , ushirikiano wa hali ya juu unahitajika miongoni mwa viongozi wa wizara, watumishi  na wadau wa sekta ya mawasiliano kwa ujumla. Aidha,Menejimenti ya wizara hiyo imetakiwa kuhakikisha kunakuwa na mazingira mazuri na wezeshi ya utendaji kazi,mahusiano bora kazini pamoja na wafanyakazi kupata stahiki zao kwa muda muafaka na pale inaposhindikana taarifa sahihi zitolewe  kwa wakati husika. Aliongeza kuwa,  kila mtumishi anatakiwa kusoma na kuelewa sera, sheria, kanuni, taratibu na miongozo mbalimbali ya utumishi wa umma na kutekeleza wajibu wao ipasavyo. “Kazi ya baraza la

WAJUMBE WA BODI YA MKURABITA WATEMBELEA KITUO JUMUISHI CHA BIASHARA NJOMBE

Image
KAMATI ya Uongozi ya Mpango wa Urasimishaji Ardhi na Biashara za Wanyonge Tanzania (Mkurabita), ikiongozwa na Mwenyekiti wa Bodi, Balozi mstaafu Daniel Ole Njoolay imetembelea Kituo Jumuishi cha Biashara kilichopo Halmashauri ya Mji wa Njombe. Walipofika katika kituo hicho walielezwa na Afisa Biashara wa Halmashauri, George Mwaseba kuhusu shughuli mbalimbali zinazofanywa katika kituo hicho ambacho kimewezeshwa na Mkurabita samani na vitendea kazi vikiwemo kompyuta 3, scanner, Printer na meza ambavyo vimerahisisha kazi na kuifanya halmashauri kuongeza mapato kupitia malipo ya leseni za biashara. Mwaseba amesema uwepo wa kituo hicho umewapunguzia usumbufu wananchi kwani sasa huduma karibu zote zinapatikana hapo. Mwenyekiti wa Bodi ya Mpango wa Urasimishaji wa Ardhi na Biashara za Wanyonge Tanzania  (Mkurabita), Balozi mstaafu Daniel Ole Njoolay (kushoto) pamoja na wajumbe wa bodi hiyo, wakipata maelezo kutoka kwa Afisa Biashara wa Halmashauri ya Mji wa Njombe, George Mwaseba  kuhusu Kitu

THUBUTU AFRICA YAANZA KUJENGA CHOO CHA KISASA SHULE YA MWAMAGUNGULI 'A' SHINYANGA

Image
  Mkurugenzi wa Shirika la Thubutu Africa Initiatives, Jonathan Manyama akisaini Mkataba wa kazi ya ujenzi wa choo cha shule ya msingi Mwamagunguli 'A' iliyopo katika kata ya Kolandoto Manispaa ya Shinyanga itakayofanywa na fundi ujenzi Robert Kayange mkazi wa kijiji cha Galamba kata ya Kolandoto.

MAJALIWA: VIONGOZI WA SEKTA YA UMMA NA BINAFSI WAENDELEZWE

Image
*Asema lengo ni kukuza ubunifu, weledi na maadili ili kuongeza tija kwa Taifa WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema viongozi wote wa Sekta za umma na binafsi wanatakiwa waendelezwe kitaaluma kwa ajili ya kukuza weledi, ubunifu na maadili ili waweze kusimamia ipasavyo maendeleo na kuongeza tija na mapato ya Taifa. Amesema katika kipindi hiki ambacho nchi imeingia katika uchumi wa kati, Serikali ingependa kuona nguvukazi katika ngazi mbalimbali inaimarishwa na kuhakikisha viongozi wanatumia ujuzi na weledi katika maeneo ya usimamizi wa rasilimali watu, rasilimali fedha na miradi. Waziri Mkuu ameyasema hayo leo (Ijumaa, Januari 29, 2021) katika Mahafali ya Wahitimu wa Programu ya Uanagenzi kwa Maafisa Watendaji Wakuu (Ceo Apprenticeship Program) yaliyofanyika katika ukumbi wa Hoteli ya Hyatt Regency, The Kilimanjaro, Dar-Es-Salaam. “Dhana ya uanagenzi ni suluhisho la kuhakikisha wataalamu wetu wanajengewa ujuzi unaohitajika mara kwa mara ili kuwaongezea umahiri katika utekelezaji wa majukum

KUTOKA MAGAZETINI LEO JUMAMOSI JANUARI 30, 2021

Image