Posts

KUTOKA MAGAZETINI LEO JUMANNE NOVEMBA 3, 2020

Image
 

DKT. HUSSEIN MWINYI AAPISHWA KUWA RAIS WA ZANZIBAR

Image
Sherehe za kumuapisha Rais mteule wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Dkt. HUSSEIN Ali Hassan Mwinyi zimefanyika leo Novemba 2, 2020 kwenye uwanja wa Aman mjini Unguja. Baada ya kula kiapo Rais Mwinyi alipokea salami ya heshima ya kupigiwa mizinga 21 kabla ya kukagua gwaride la heshima la vikosi vya ulinzi na usalama. Katika hafla hiyo iliyofana, vingozi mbalimbali wa Bara na Zanzibar wakiwemo wastaafu walihudhuria hafla hiyo bapo Rais aliyemaliza muda wake wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Dkt. Ali Mohammed Shein na mkewe mama Mwanamwema Shein walihudhuria hafla hiyo.  

RAIS MHE. DKT. MAGUFULI AKABIDHIWA CHETI CHA USHINDI NA TUME YA TAIFA YA UCHAGUZI NEC MARA BAADA YA KUTANGAZWA MSHINDI WA KITI CHA URAIS KATIKA UCHAGUZI MKUU ULIOFANYIKA TAREHE 28 OKTOBA 2020

Image
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akionesha Cheti cha Ushindi wa Kiti cha Urais alichokabidhiwa na Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Jaji Mstaafu Semistocles Kaijage mara baada ya kutangazwa mshindi kwa Kiti cha Urais katika Uchaguzi Mkuu uliofanyika tarehe 28 Oktoba 2020. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akipokea Cheti cha Ushindi wa Kiti cha Urais kutoka kwa Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Jaji Mstaafu Semistocles Kaijage mara baada ya kutangazwa mshindi kwa Kiti cha Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Uchaguzi Mkuu uliofanyika tarehe 28 Oktoba 2020, hafla hiyo ya kukabidhiwa Cheti imefanyika katika Makao Makuu ya Tume ya Uchaguzi NEC Njedengwa jijini Dodoma leo tarehe 01 Novemba 2020. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Wageni mbalimbali waliofika katika hafla fupi ya kukabidhiwa Cheti cha Kiti cha Urais wa

KUTOKA MAGAZETINI LEO JUMATATU NOVEMBA 2, 2020

Image

KUTOKA MAGAZETINI LEO JUMAPILI NOVEMBA 1, 2020

Image