WADAU WA NYAMA WENYE MABUCHA WATAKIWA KUCHANGAMKIA FURSA ZA MIKOPO YA VIFAA VYA KISASA VYA KWENYE MABUCHA
Kaimu Msajili Bodi ya Nyama Tanzania huyo aliyevaa (koti la suti) Imani Sichalwe akiwa na viongozi wa wadau wa Nyama Arusha,viongozi wa kampuni ya watertras na viongozi wa Amana benki. Kaimu Msajili Bodi ya Nyama Tanzania huyo aliyevaa (koti la suti) Imani Sichalwe akikagua moja ya mashine za kisasa za kukatia nyama vitakavyosambazwa na Kampuni ya watertras Na Vero Ignatus. Wadau wa Nyama Nchini watakiwa kujiunga Kwenye vikundi na visajiliwe kwa mujibu wa sheria ,Jambo litakalowawezesha kuwa na Vigezo vya kukopesheka kwenye Taasisi mbali mbali za kifedha Nchini. Hayo yamesemwa na Kaimu Msajili wa Bodi ya Nyama Nchini Tanzania Imani Sichalwe ,mara baada ya kumalizika kikao kazi kilichofanyika mkoani Arusha kikihusisha viongozi wa Amana bank, viongozi wa wauzaji nyama Arusha, viongozi wa kampuni ya watertrans Lengo likiwa ni kujadili na kukubaliana kwa pamoja ni namna gani wauzaji nyama Kwenye mabucha wanaweza kukopesheka. Sichalwe amesema ni muda mrefu wadau wa nyama ,wa