WAKAZI 60,000 BABATI KUPATA MAJISAFI NA SALAMA
Jumla ya wakazi 60,000 wa Mji wa Magugu Wilayani Babati Mkoani Manyara wanatarajia kunufaika na huduma ya maji pindi mradi wa maji unaotekelezwa kwa kutumia chanzo cha Mto Kou utakapokamilika. Hayo yameelezwa Septemba 27, 2020 wakati wa ziara ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji, Mhandisi Anthony Sanga wilayani humo ya kukagua hatua ya utekelezaji wa mradi huo na Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Babati (BAWASA), Mhandisi Idd Msuya. Mara baada ya kupokea taarifa na kujionea hali halisi ya hatua iliyofikiwa ya utekelezwaji wa mradi, Mhandisi Sanga aliielekeza BAWASA kufanya mapitio ya mradi kwenye baadhi ya maeneo ili kuongeza tija. “Hakikisheni mtandao wa maji unaongezeka ili muweze kuwafikia wananchi wengi zaidi lakini pia wananchi waweze kunufaika kwa Saa 24 kila siku,” alielekeza Mhandisi Sanga. Aidha, Katibu Mkuu Sanga aliielekeza BAWASA kuhakikisha mradi huo wa Magugu unakamilika kwa wakati na kwamba jitihada zifanyike ili utekelezwaji wake ufanyike bil