Posts

DKT. BITEKO ATEMBELEA BANDA LA NSSF MAONESHO YA OSHA

Image
Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Dotto Biteko (wapili kulia), akimsikiliza Meneja Uhusiano na Elimu kwa Wanachama, Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF), Lulu Mengele alipotembelea banda la Mfuko huo, kwenye Maonesho ya Afya na Usalama Mahali pa Kazi (OSHA), katika uwanja wa General Tyre, Njiro jijini Arusha, Aprili 28, 2024. NSSF, inashiriki katika maonesho hayo ili kutoa fursa kwa wananchi kuweza kupata taarifa kuhusu shughuli zinazotekelezwa na Mfuko huo. Maonesho ya mwaka huu 2024, yamebeba kauli mbiu isemayo, “Athari za mabadiliko ya tabia nchi katika usalama na afya kazini; Sajili eneo la kazi OSHA katika harakati za kupunguza athari hizo.” Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Dotto Biteko (katikati), akizungumza jambo wakati alipotembelea banda la NSSF, kwenye Maonesho ya Afya na Usalama Mahali pa Kazi (OSHA), katika uwanja wa General Tyre, Njiro jijini Arusha, Aprili 28, 2024. Wengine pichani ni Naibu Waziri wa Nchi Ofisis ya Waziri Mkuu (Kazi,

NAIBU WAZIRI MKUU DKT. BITEKO AWAPA KONGOLE WCF

Image
NA K-VIS BLOG/KHALFAN SAID, ARUSHA NAIBU Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Dotto Biteko, ameupongeza Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF) kwa kazi nzuri unayofanya katika kuwahudumia wadau wake. Mhe. Dkt. Biteko ametoa kauli hiyo alipotembelea banda la WCF kwenye Maonesho ya Wiki ya Usalama na Afya Mahali pa Kazi yanayoendelea kwenye viwanja vya General Tyre, Njiro jijini Arusha. “Hongereni kwa kazi nzuri mnayofanya, nimeona jinsi mnavyoendelea kutoa elimu kuhusu shughuli za Mfuko, juzi niliona mlikuwa na Waheshimiwa Mabalozi wetu mkiwapa elimu, hongereni sana,” alisema Dkt. Biteko. Aidha, Dkt. Biteko ametoa maelekezo kwa Mkurugenzi Mkuu wa WCF, Dkt. John Mduma kuyatumia maonesho hayo kama sehemu ya kutoa elimu zaidi kwa wananchi wanaotembelea maonesho hayo . Akitoa hotuba kwenye maadhimisho hayo Mhe Dkt. Biteko, amesisitiza umuhimu wa waajiri na waajiriwa kuzingatia usalama na afya mahali pa kazi. “Hakikisheni mnakuwa kwenye mazingira mazuri ya kazi ili wakati wote tuweze ku

SERIKALI YATOA BIL 1.5 UREJESHAJI MIUNDOMBINU YA BARABARA MWANZA

Image
Serikali imetoa shilingi Bilioni 1.5 kwa ajili ya kuanza urejeshaji wa miundombinu ya barabara zilizoharibika maeneo mbalimbali Mkoani Mwanza. Fedha hizo zimetolewa na serikali kwenda Wakala ya Barabara Tanzania (TANROADS) Mkoa wa Mwanza ili kuanza haraka kazi ya marekebisho miundombinu ya barabara na madaraja ambayo yameharibika kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha Meneja wa TANROADS Mkoa Wa Mwanza Mhandisi Paschal Ambrose ameyasema hayo wakati alipotembelea na kukagua uharibifu uliotokea kwenye barabara katika Wilaya za Nyamagana na Misungwi ambapo pia ametumia fursa hiyo kukanusha uvumi ulioenezwa kwamba barabara katika eneo la Ng'ombe Wilayani Misungwi ni mbovu na haipitiki na amewataka wananachi kupuuza uvumi huo. Amesisitiza kuwa Serikali imetoa fedha za dharura ambapo tayari wakandarasi wapo kazini wakiendelea na kazi. Amesema miongoni mwa barabara zinazofanyiwa marekebisho ni barabara ya kutoka Mwanza kuelekea Musoma eneo la Nyamhongolo ambapo wanarekebisha mfereji amba

RAIS SAMIA AKUTANA NA RAIS MOHAMUD WA SOMALIA

Image
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha ya pamoja na Mgeni wake Rais wa Shirikisho la Jamhuri ya Somalia Mhe. Dkt. Hassan Sheikh Mohamud mara baada ya kuwasiliIkulu Jijini Dar es Salaam kwa ziara ya Kiserikali tarehe 27 Aprili 2024. Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan na Mgeni wake Rais wa Shirikisho la Jamhuri ya Somalia Mhe. Dkt. Hassan Sheikh Mohamud wakizungumza na Waandishi wa Vyombo mbalimbali vya Habari mara baada ya Mkutano wao uliofanyika katika ukumbi wa Jakaya Kikwete, Ikulu Jijini Dar es Salaam Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiongoza Ujumbe wa Tanzania kwenye mazungumzo ya pamoja na Mgeni wake Rais wa Shirikisho la Jamhuri ya Somalia Mhe. Dkt. Hassan Sheikh Mohamud na Ujumbe wake yaliyofanyika katika ukumbi wa Jakaya Kikwete, Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 27 Aprili, 2024. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiongoza Ujumbe wa Tanzania kwenye mazungumzo ya pamoja na Mge

SERIKALI ITAENDELEA KUSHIRIKIANA NA SHULE BINAFSI- DKT. BITEKO

Image
Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko amesema kuwa Serikali itaendelea kushirikiana na sekta binafsi hususan shule binafsi ili kuboresha sekta ya elimu nchini. Akizungumza katika Mkutano Mkuu wa Chama cha Wamiliki wa Shule Binafsi Nchini (TAPIE), leo Aprili 27, 2024 jijini Dar es salaam Dkt. Biteko amesema kuwa Serikali inayoongozwa na Dkt. Samia Suluhu Hassan haiwezi kuacha Wadau wa Elimu wakilalamika, kwa kuwa uwepo wao unaisaidia Serikali. “Nataka niwahakikishie kuwa Serikali imeendelea kukutana na TAPIE mara kwa mara, na hapa namuelekeza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge na Uratibu, Mhe. Jenista Mhagama kuratibu mkutano wa pamoja kati ya TAPIE na Wizara za Ardhi, Fedha, Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji na Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) ili kujadiliana kwa pamoja na kupata suhulu ya changamoto zinazowakabili”, amesema Dkt. Biteko. Katika hatua nyingine, Dkt. Biteko amewaasa TAPIE kuzingatia masharti yaliyoaini

DKT. MERU ATEMBELEA BANDA LA NSSF MAONESHO YA OSHA 2024 ARUSHA

Image
Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini, Mamlaka ya Usalama na Afya Mahali pa Kazi (OSHA), Dkt. Adelhem J. Meru (kushoto), akipatiwa maelezo na Meneja Uhusiano na Elimu kwa Wanachama NSSF, Lulu Mengele kuhusu shughuli zinazofanyika katika banda la Mfuko huo katika Maonesho ya Wiki ya Usalama na Afya Mahali pa Kazi, kwenye viwanja vya General Tryre, Njiro jijini Arusha, Aprili 27, 2024. NSSF inashiriki katika maonesho hayo ili kutoa fursa kwa wananchi kuweza kupata elimu ya hifadhi ya jamii, ikiwa ni pamoja na kuwahudumia wanachama wa Mfuko huo. Maonesho ya mwaka huu 2024 yamebeba kauli mbiu isemayo, “Athari za mabadiliko ya tabia nchi katika usalama na afya kazini; Sajili eneo la kazi OSHA katika harakati za kupunguza athari hizo.”