NA K-VIS BLOG/KHALFAN SAID, ARUSHA MFUKO wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF), umewakumbusha wanachama wake kuwa, huduma zote zinazohusiana na uanachama wa mwanachama zinapatikana mtandaoni, (PSSSF Kiganjani). Meneja wa PSSSF, Kanda ya Kaskazini, Bi. Vonness Koka, amesema hayo wakati akiongoza timu ya watumishi wa Mfuko huo kupeleka elimu ya matumizi ya PSSSF Kiganjani kwenye mabanda ya maonesho ya Wiki ya Usalama na Afya Mahali pa Kazi (OSHA), kwenye viwanja vya General Tyre jijini Arusha Aprili 25, 2025. “Tumeanzisha mfumo wa PSSSF Kiganjani unaomuwezesha mwanachama kupata taarifa za Michango yake mahali popote alipo bila ya kufika kwenye ofisi zetu, vile vile mfumo unamuwezesha mstaafu kujihakiki akiwa nyumbani kwake, safarini au mahali popote. Tunawakaribisha wanachama wote waliopo Kilimanjaro, Manyara, Tanga, Arusha na wananchi kwa ujumla, kufika kwenye banda letu ili kupata elimu hiyo ya matumizi ya PSSSF Kiganjani.” Amefafanua Bi. Koka. Amesema, kupitia si