VIJANA JKT WAPONGEZWA KWA KUONESHA UZALENDO MSOMERA
VIJANA wanaoshiriki kwenye kazi mbalimbali za ujenzi katika Kijiji cha Msomera wamepongezwa kutokana na kufanya kazi kwa kujituma na kuonesha uzalendo kwa taifa ili kufanikisha mpango wa serikali wa kuwahamisha wananchi kwa hiyari kutoka ndani ya Hifadhi ya Ngorongoro. Akizungumza mara baada ya kamati ndogo ya ulinzi na usalama kutembelea eneo hilo Makamu Mwenyekiti wa Kamati hiyo Kamishna wa Polisi Charles Mkumbo amesema vijana hao ambao wanashiriki katika kazi hizo wameonesha uzalendo mkubwa katika kutimiza majukumu yao kwa maslahi ya taifa. Amesema zoezi la ujenzi wa nyumba linalofanywa na Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania kupitia SUMA-JKT limeonesha mafanikio makubwa ambapo kwa mujibu wa taarifa ya jeshi hilo ujenzi wa nyumba 2559 katika Kijiji cha Msomera linatarajiwa kumalizika mwishoni mwa mwezi ujao. Mapema Mkuu wa Wilaya ya Handeni Mheshimiwa Albert Msando amesema pamoja na jeshi hilo kufanya kazi vizuri changamoto kubwa kwa sasa ni kwa baadhi ya Wizara za kisekta ku