Posts

KUTOKA MAGAZETINI NOVEMBA 28, 2023

Image
 

WITO WATOLEWA KWA WATAFITI KUFANYA TAFITI ZENYE TIJA

Image
  Wito umetolewa kwa watafiti na wanataaluma nchini kujikita katika kufanya tafiti zenye tija  kwa Taifa  na zinazoleta majawabu kwenye changamoto  zinazoikabili jamii inayowazunguka. Wito huo umetolewa leo na Naibu Mkuu wa Chuo cha Uhasibu Arusha (IAA) Taaluma, Utafiti na Ushauri wa Kitaalam, Prof. Epaphra Manamba; alipomwakilisha Mkuu wa Chuo katika ufunguzi wa Kongamano la Kitaaluma la Vitivo linalowahusisha wanataaluma na wanafunzi wa shahada ya Uzamili IAA katika kuwasilisha tafiti zao, machapisho na kufanya mijadala ya kina.  Prof. Manamba amesema kupitia kongamano hilo wanafunzi wamewasilisha tafiti zinazolenga kuangalia Taifa kwa baadaye kwenye maeneo ya Uchumi,Bima,Utalii, Fedha, TEHAMA. Uongozi, Biashara na maeneo mengine, ili jamii iweze kuzipokea na  kutatua matatizo yanayowakabili kulingana na matokeo ya tafiti husika. “Ni takwa la IAA kila mwanafunzi anayesoma shahada ya uzamili  kufanya utafiti  na kuwasilisha au kuwa na chapisho katika majarida ya kitaifa na Kimataifa,j

VYAMA VYA SIASA VYAONESHA USHIRIKIANO UBORESHAJI DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA TABORA

Image
    Mkazi wa Kata ya Ng'ambo aliyefika katika Kituo cha Kizigo Mzee Juma Rai  Juya, akionesha kadi yake ya mpiga kura mara baada ya kukamilisha taratibu za kuboresha taarifa zake kwenye daftari la wapiga kura na Kukabidhiwa kadi yake mpya. Afisa Mtendaji wa kata  na  Mwandikishaji Msaidizi Kata ya Ng'ambo, Rehema Midelo akizungumza na mwandishi wetu katika kituo cha Masempele kata ya Ng'ambo mjini Tabora wakati akielezea namna zoezi hilo linavyoenda kwa ufanisi mkubwa. Wakala wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Kituo Cha Kaze Shule ya Sekondari, Bw. Brayson Dickson akielezea namna zoezi la uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wazpiga kura linavyoendelea katika kituo cha Shule ya Sekondari Kaze mjini Tabora. Bi Leila Muhaji Kaimu Mkurugenzi Masidizi Habari kutoka Tume ya Taifa ya Uchaguzi kulia akifuatilia zoezi la uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura katika kituo cha Kizigo kata ya Ng'ambo mkoani Tabora. ........................... Vyama vya Siasa pamoja na Wakazi