Posts

KUTOKA MAGAZETINI OKTOBA 30, 2023

Image
 

WAZIRI KAIRUKI KUFUNGUA MKUTANO WA KAMISHENI YA MISITU NA WANYAMAPORI YA AFRIKA

Image
  Na John Mapepele Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Angellah Jasmin Kairuki (Mb) anatarajiwa kuwa Mgeni Rasmi kwenye mkutano wa 24 wa Kamisheni ya Misitu na Wanyamapori ya Afrika utakaofanyika kuanzia jijini Arusha kesho Oktoba 30 hadi Novemba 3, 2023. Kwa mujibu wa taarifa ya Wizara ya Maliasili na Utalii iliyosainiwa na Mhe. Kairuki, Mkutano huo utafanyika sambamba na Wiki ya Misitu na Wanyamapori ya Afrika ya Nane (AFWW8) katika Hoteli ya Gran Melia jijini Arusha, Tanzania. Serikali ya Tanzania, kwa kushirikiana na Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa (FAO), itakuwa mwenyeji wa Mkutano wa Ishirini na Nne (24) wa Kamisheni ya Misitu na Wanyamapori Afrika (AFWC24) Taarifa hiyo imefafanua kuwa Kamisheni ya Misitu na Wanyamapori ya Afrika (AFWC) ni moja ya Kamisheni sita za Misitu za Kikanda za FAO, ikiwa ni mamlaka ya kisheria ya juu ya Afrika katika masuala ya misitu na wanyamapori. Ni jukwaa maalum ambapo viongozi wa misitu na wanyamapori kutoka nchi wanachama wa Afrik

KUTOKA MAGAZETINI OKTOBA 29, 2023

Image