RAIS SAMIA AZINDUA MIRADI MBALIMBALI YA MAENDELEO KUELEKEA KWENYE KILELE CHA TAMASHA LA KIZIMKAZI ZANZIBAR
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akikagua Kituo cha Afya cha mama na mtoto Kizimkazi Dimbani tarehe 29 Agosti, 2023 mara baada ya kukizindua katika shamrashamra za kuelekea kwenye kilele cha Tamasha la Kizimkazi Mkoa wa Kusini Unguja. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa pamoja na viongozi wengine wakati akikata utepe kufungua Chumba cha Kompyuta na ukumbi wa Mtihani wa Skuli ya Sekondari ya Muyuni B kwenye hafla fupi iliyofanyika Mkoa wa Kusini Unguja Zanzibar katika shamrashamra za kuelekea kwenye kilele cha Tamasha la Kizimkazi tarehe 29 Agosti, 2023. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza wakati akikagua Madarasa ya Shule ya Msingi Muyuni B mara baada ya ufunguzi katika Mkoa wa Kusini Unguja Zanzibar tarehe 29 Agosti, 2023. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akikata utepe kuzindua ugawaji wa Gari la OCD Kizimkazi Mkunguni pamoja na Gari la OCD Makund