WAISLAM SINGIDA WAPONGEZA ZOEZI LA UGAWAJI NYAMA SADAKA YA CHINJA
Na Dotto Mwaibale, Singida WAISLAM Singida wamepongeza utaratibu uliotumika kugawa wanyama waliochinjwa kwa ajili ya kusherehekea Sikukuu ya Eid Ul Adha ambayo inafanyika leo duniani kote. Wakizungumza kwa nyakati tofauti wakati wa ugawaji wa wayama hao mjini hapa walisema zoezi hilo kwa mwaka huu limeratibiwa vizuri kwani waislam na wananchi wengi wamepata sadaka hiyo tofauti na mwaja ambapo licha ya wanyama hao kuwa wengi kulikuwa na ujanja ujanja uliosababisha wengi wao kukosa. Mkazi Mungumaji katika Manispaa ya Singida, Amina Hamadi alipongeza utaratibu uliofanyika wa ugawaji wa sadaka hiyo kwa kusema mwaka jana hakupata kabisa licha ya kuwepo jirani na kambi ya uchinjaji maeneo ya Karakana. “Mwaka jana nilishinda kutwa nzima nikiwa na wenzangu lakini hatukupata sadaka hii lakini leo tumepata mbuzi mmoja tugawane watu wawili jambo ambalo sikulitegemea kabisa,” alisema Amina. Abubakar Ntandu aliyekuwepo kwenye zoezi hilo alisema utaratibu uliofanywa na Taasisi ya uchinjaji wa wafany