Posts

KUTOKA MAGAZETINI LEO JUMATANO MEI 31, 2023

Image
 

WATENDAJI WA OFISI YA MAKAMU WA PILI WA RAIS ZANZIBAR KUTEMBELEA MIRADI YA TASAF UTETE RUFIJI

Image
  Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF, Ladislaus Mwamanga (katikati) akizungumza na Watendaji kutoka Ofisi ya Makamu wa pili wa Rais wa Wanzibar na watendajiwa TASAF kutoka visiwani humo, walipotembelea ofisi za TASAF Dar es Salaam wakiwa njiani kwenda Halmashauri ya Wilaya ya Rufiji kwa ziara ya mafunzo Jumanne Mei 30, 2023. Kutoka kulia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Usimamizi wa Miradi ya TASAF Mwajuma Mussa Ali, Kaimu Sheha wa Kizimkazi Kasim Fadhili Ramadhan, Mratibu wa TASAF Unguja Makame Ali Haji na Meneja wa Uratibu na Itifaki wa TASAF, Tunu Munthali. Bw Mwamanga aliwapongeza watendaji hao kwa kazi nzuri na kuwataka kuhamasisha wanufaika waliofanikiwa kujikwamua kuichumi kukubali kuondolewa kwenye Mpango wa Kunusuru Kaya za Walengwa kwa hiari yao ili kuwapa nafasi wengine kunufaika. Watendaji hao wako katika ziara ya siku mbili katika Halmashauri ya Wilaya ya Rufiji kujifunza usimamizi wa miradi ya TASAF Kaimu Sheha wa Kizimkazi Kasim Fadhili Ramadhan Katika Ofisi za TASAF wakati wate

PSSSF YAPEWA TUZO YA KIMATAIFA

Image
  NA K-VIS BLOG/KHALFAN SAID, DAR ES SALAAM MFUKO wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF) Umepewa tuzo na Taasisi ya Kimataifa ya Hifadhi ya Jamii (International Social Security Association-ISSA)kutokana na mafanikio iliyoyapata katika kipindi kifupi baada ya kuunganishwa (Merge) kwa mifuko minne ya Hifadhi ya Jamii ya PSPF, PPF, GEPF NA LAPF na kuwa PSSSF. Akizungumzia tuzo hiyo, Mkurugenzi Mkuu wa PSSSF, CPA. Hosea Kashimba alisema sababu nyingine iliyoifanya ISSA kutoa tuzo kwa Mfuko huo ni pamoja na jinsi Mfuko ulivyoweza kupunguza gharama za uendeshaji na ulipaji wa mafao kwa wakati. “Kwenye suala la kuunganisha mifuko yapo mambo manne ambayo ISSA imeyaona na kuona ni mafanikio ambayo ni pamoja na kupunguza gharama za uendeshaji, kutoa mafao yanayofanana kwa wanachama wa Mfuko licha ya kutoka kwenye mifuko tofauti, kukabiliana na madeni kabla ya mifuko kuunganishwa na pia suala la uwekezaji hususan katika viwanda.” Alisema CPA Kashimba aliishukuru Bodi ya Wadhami

WARIRI MAZRUI AKUTANA NA MKUU WA WHO DKT. TEDROS ADHANOM GHEBREYESUS, AIPONGEZA TANZANIA KWA UDHIBITI MAGONJWA YA MLIPUKO

Image
Ujumbe wa Tanzania ukiongizwa na Waziri wa Afya Serikali ya Mapinduzi  Zanzibar Mhe. Nassor Mazrui umekutana na kufanya mazungumzo na Mkurugenzi Mku wa Shirika la Afya Duniani (WHO) Dkt. Tedros Adhanom Ghebreyesus pembezoni mwa Mkutano Mkuu wa 76 wa Shirika la Afya Duniani (WHA76) Geneva Uswis. Katika mazungumzo hayo, Mkurugenzi Mkuu wa WHO, Dkt. Tedros Adhanom Ghebreyesua ameipongeza  Tanzania kwa jududi inazoendelea kufizanya katika kupambana na kudhibiti magonjwa ya mlipuko kuingia na kuenea nchini. Waziri wa AfyaSerikali ya Mapinduzi   Zanzibar Mhe.Nassor Mazrui akiwa katika picha na  Mkurugenzi Mku wa Shirika la Afya Duniani (WHO) Dkt Tedros Adhanom Ghebreyesus huko Geneva Kikao cha ujumbe wa Tanzania na Mkurugenzi Mkuu wa WHO,  Dkt Tedros Adhanom Ghebreyesus Mganga Mkuu wa Serikali Prof. Tumaini Nagu akipeana mikono na Mkurugenzi Mkuu wa WHO, Dkt. Tedros Adhanom Ghebreyesus Dkt Tedros Adhanom Ghebreyesus, Waziri Mazrui katika picha ya pamoja na ujumbe mzima wa Tanzania na maafisa

KUTOKA MAGAZETINI LEO JUMANNE MEI 30, 2023

Image