CHAMA CHA WASTAAFU WA BENKI KUU YA TANZANIA (BOTRA) WAKUTANA KUJADILI MIKAKATI, KUPITISHA MPANGO KAZI 2023.
Mwenyekiti wa Chama Cha Wastaafu wa Benki Kuu ya Tanzania (BOTRA) Bi. Grace Rubambe akifungua mkutanomkuu wa mwaka wa chama hicho uliofanyika kwenye ukumbi wa BoT jijini Dar es Salaam Aprili 27,2023. ................................................... NA JOHN BUKUKU, DAR ES SALAAM. Wafanyakazi wa sekta ya umma na binafsi nchini wametakiwa kuwa na utamaduni wa kujiandaa mapema kustaafu kwa kutengeneza mazingira rafiki ya kiuchumi jambo ambalo litawasaidia kuishi maisha ya heshimu katika jamii kipindi wanapostaafu. Akizungumza lo tarehe 27/4/2023 Jijini Dar es Salaam katika Mkutano Mkuu wa Mwaka, Mwenyekiti wa Chama Cha Wastaafu wa Benki Kuu ya Tanzania (BOTRA) Bi. Grace Rubambe, amesema mkutano mkuu huo umelenga kufanya uchaguzi wa viongozi, kujadili mpango mkakati, Bajeti pamoja na kupitisha mpango kazi wa mwaka 2023. "Tunatarajia katika mkutano huu kuchangua viongozi watakaotuongoza katika kipindi cha miaka mitatu ijayo" amesema Bi. Rubambe. Bi. Rubambe amesema kuwa