Posts

MAKAMU WA RAIS WA MAREKANI KAMALA HARRIS AWASILI NCHINI

Image
 Matukio mbalimbali  yakionyesha Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango akimpokea Makamu wa Rais wa Marekani Mhe. Kamala Harris alipowasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es salaam usiku wa kuamkia leo Machi 30, 2023 akianza ziara ya kikazi ya siku tatu nchini.

WAZAZI NA WALEZI WANAWAJIBU WA KUSIMAMIA MAADILI KWA WATOTO NA VIJANA NCHINI

Image
 Na Eleuteri Mangi, WUSM - Dar es Salaam Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Utamaduni, Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Emmanuel Temu amewataka wazazi/walezi kusimamia ipasavyo suala la maadili nchini kulingana na Utamaduni wa Mtanzania. Dkt. Temu ametoa wito huo Machi 29, 2023 akiwa katika kipindi cha Jambo Tanzania kinachorushwa kupitia Televisheni ya Taifa, TBC1 Mikocheni jijini Dar es Salaam. "Wazazi tunawajibu wa kuwaunganisha watoto wetu na Utamaduni wao, miaka ya nyuma watoto walifundishwa masuala ya unyago, jando, hadithi za nyumbani Kila mara jioni ili kuwafunda watoto na vijana wetu.wathamini Utamaduni wetu" amesema Dkt. Temu. Dkt. Temu amesema Viongozi Wakuu wa Kitaifa Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan, Makamu wa Rais Dkt. Philip Mpango na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa wapo mstari wa mbele kusisitiza kulinda, kusimamia na kurejesha maadili ya Mtanzania na kusisitiza kuwa  Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo ipo mstari wa mbele kutekeleza maelekezo ya Viongo

RAIS SAMIA APOKEA TAARIFA YA TAASISI YA KUZUIA NA KUPAMBANA NA RUSHWA-TAKUKURU PAMOJA NA TAARIFA YA OFISI YA MKAGUZI MKUU WA HESABU ZA SERIKALI (CAG) KWA MWAKA WA FEDHA 2021-2022

Image
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akipokea Taarifa ya Ofisi ya Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali kwa mwaka 2021/2022 kutoka kwa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali Bw. Charles Kichere, Ikulu Jijini Dar es salaam tarehe 29 Machi, 2023. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akipokea Taarifa ya Taasisi ya Kupambana na Kuzuia Rushwa (TAKUKURU) kwa mwaka 2021/2022 kutoka kwa Mkurugenzi wa Taasisi hiyo CP. Salum Hamduni Ikulu Jijini Dar es salaam tarehe 29 Machi, 2023. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Viongozi mbalimbali mara baada ya kupokea Taarifa ya Ofisi ya Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) na Taarifa ya Taasisi ya Kupambana na Kuzuia Rushwa (TAKUKURU) kwa mwaka 2021/2022, Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 29 Machi, 2023. Kutoka kulia Makamu wa Rais Mhe. Dkt. Philip Mpango, Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa, Spika wa Bunge Mhe. Dkt. Tulia Ackson, Jaji Mkuu Mhe. Prof

KATIBU MKUU WA CCM, NDG. DANIEL CHONGOLO ALIPOHUTUBIA KIKAO KAZI CHA 18 CHA TAGCO

Image
Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Ndg. Daniel Chongolo akizungumza kwenye Kikao Kazi cha 18 cha Maafisa Habari, Mawasiliano na Uhusiano kutoka Serikalini (TAGCO) kwenye Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNICC) jijini Dar es Salaam Machi 29, 2023. Kikao hicho cha siku tano kimebeba kauli mbiu isemayo "Mawasiliano ya Kimkakati Injini ya Maendeleo".  (PICHA NA K-VIS BLOG/KHALFAN SAID). Katibu wa TAGCO, Bw. Abdul Njaidi (wapili kulia) na baadhi ya wajumbe wengine wa Kamati ya Utendaji ya TAGCO, wakisikiliza hotuba ya Ndg. Chongolo. Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhe. Nape Nnauye, akizungumza kwenye Kikao hicho. Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhe. Nape Nnauye, akizungumza kwenye Kikao hicho. Mwenyekiti wa TAGCO, Bi. Sarah Kibonde Washiriki wakifuatilia kwa makini hotuba ya Katibu Mkuu wa CCM, Ndg. Daniel Chongolo ( hayupo pichani). Katibu Mkuu wa CCM, Ndg. Daniel Chongolo (kulia) akiteta jambo na Waziri wa

MAAFISA HABARI WA SERIKALI (TAGCO); TAIFA STARS BADO INA NAFASI YA KUFUZU AFCON2023 LICHA YA KUPOTEZA MBELE YA UGANDA CRANES

Image
  NA K-VIS BLOG/KHALFAN SAID LICHA ya timu ya soka ya Taifa, Taifa Stars, kupoteza pambano lake la marudiano la michuano ya kutafuta nafasi ya kufuzu kucheza fainali ya AFCON2023 kwa kufungwa bao 1-0 na timu ya Taifa ya Uganda, (The Cranes), Maafisa Habari, Mawasiliano na Uhusiano Serikalini (TAGCO) bado wana matumaini ya Stars kufuzu michuano hiyo. Wameyasema hayo mara baada ya kumalizika kwa pambano hilo lililopigwa kwenye uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam usiku wa kuamkia leo Machi 29, 2023. Maafisa habari hao wapatao 600 kutoka Tanzania Bara na Tanznaia Zanzibar ambao wanashiriki Kikao Kazi jijini Dar es Salaam, walikuwa ni miongoni mwa mamia ya mashabiki wa soka waliofurika uwajani hapo kuipa hamasa timu yetu ya Taifa. Maafisa hao ambao ni miongoni mwa watanzania waliopata ofa ya tiketi 7,000 zilizonunuliwa na Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa wapenzi wa soka, walishangilia kwa muda wote bila kuchoka hadi ilipofika dakik

TAA INATHAMINI MICHEZO KWA WATUMISHI-DG MBURA

Image
  Katibu Mkuu wa Klabu ya Michezo ya Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi (Sekta ya Uchukuzi), Bw. Mbura Tenga (kulia), akimkabidhi kombe la ushindi wa jumla , Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya ndege Tanzania (TAA) walilolipata kutoka kwenye michezo ya Shirikisho la Michezo ya Wizara na Idara za Serikali (SHIMIWI), pia michezo ya Mei Mosi na mabonanza. Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya ndege Tanzania, Bw. Mussa Mbura (wa kwanza kushoto) akimsikiliza Katibu Mkuu wa Klabu ya Michezo ya Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi (Sekta ya Utamaduni), Bw. Mbura Tenga (kulia), akitoa historia fupi ya klabu hiyo, kwenye hafla ya kukabidhiwa vikombe vya ushindi wa michezo ya Shirikisho la Michezo ya Wizara na Idara za serikali (SHIMIWI), Mei Mosi na mabonanza. Baadhi ya wanamichezo wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), wakiwa kwenye picha ya pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka hiyo, Bw. Mussa Mbura (watano kutoka kulia), baada ya kukabidhi vikombe vya ushindi wa michezo ya Shirikisho la

KUTOKA MAGAZETINI LEO JUMATANO MACHI 29, 2023

Image